Home Michezo KIFARU: ETI NINI, HUMUD BADO NI MALI YA MTIBWA NA HAENDI KOKOTE

KIFARU: ETI NINI, HUMUD BADO NI MALI YA MTIBWA NA HAENDI KOKOTE

0

***********************************

Licha ya tetesi za kutakiwa na klabu ya Yanga Uongozi wa Mtibwa Sugar umefunguka kuwa kiungo wao Abdulhalim Humud haendi popote.

Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru amesema kiungo huyo ni mchezaji muhimu na ana mkataba hivyo ataendelea kuhudumu katika kikosi hicho chenye makazi yake mkoani Morogoro.

Kifaru amesema kiungo huyo alipokuwa anacheza moja ya timu kubwa za hapa jijiji Dar es Salaam alionekana hana kitu lakini baada ya kumrudisha Mtibwa wanataka kumchukua tena. “Humud anapata kila kitu hapa na hataenda popote bado ana mkataba na Mtibwa haitakuwa tayari kuona akiondoka,” alisema Kifaru.

Kwa vipindi tofauti Humud amewahi kuzichea timu za Azam FC na Simba hivyo kama atafanikiwa kujiunga na Yanga atakamilisha kuzichezea timu zote kubwa za hapa jijini.