Home Siasa TLP kumuumga mkono Rais JPM kwenye Uchaguzi Mkuu

TLP kumuumga mkono Rais JPM kwenye Uchaguzi Mkuu

0

*************************************

Chama Cha Tanzania Labour Party-TLP kupitia Mkutano Mkuu wake uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo umekubaliana kutosimamisha mgombea Urais kupitia chama hicho na kumuunga mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza wakati akitoa maazimio ya Mkutano Mkuu wa TLP M/kiti wa TLP Bw.Agustine Lyatonga Mrema amesema wamefikia maazimio hayo kutokana na kazi kubwa aliyoifanya JPM katika miaka 5 ya awali ya kuwatumikia wananchi kwa weledi,haki na wajibu na kuelezea kuwa chama hicho kitakuwa tayari kusimama katika majukwaa kuelezea kazi kubwa Iliyofanywa na Rais Magufuli.

Aidha Bw. Mrema amesema TLP hakitakuwa tayari kuwa sehemu ya vyama vinavyotumika na wasioitakia mema nchi na kueleza wasiwasi wake katika kuungana na vyama vingine kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Naye Katibu Mwenezi wa CCM Bw.Humphrey Polepole akiongea katika mkutano hup akimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, amekipongeza TLP kwa uamuzi wake wa kumuunga Mkono Dkt. Magufuli lakini pia kwa ukomavu katika demokrasia.

Wakati huo huo Bw.Pole pole amewataka Watanzania kuendelea kufanya kazi na kuondokana na hofu wakati wakiendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.