Home Mchanganyiko Ujenzi wa maabara ya kisasa ya upasuaji ubongo wakamilika kwa asimia 70

Ujenzi wa maabara ya kisasa ya upasuaji ubongo wakamilika kwa asimia 70

0

Bw. Abraham Okero kutoka kampuni ya Pyramid akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile ya namna mitambo ya maabara ya kisasa ya upasuaji wa ubongo itakavyafanya kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa taarifa kuhusiana na hatua ya ujenzi wa mradi wa maabara ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo (Angio suite) ambao umekamilika kwa asilimia 70%

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Dkt Faustine Ndugulile akitoa maelekezo katika chumba cha teleradiolojia kinachotarajiwa kufanyiwa majaribio siku ya ijumaa tarehe 05/05/2020.

***************************************

Serikali imeelezwa kwamba ujenzi wa maabara ya kisasa ya upasuaji wa ubongo (Angio Suite) umekamilika kwa asilimia 70 na kwamba itaanza kutumika wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Dkt. Respicious Boniface wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile alipoitembelea taasisi hiyo kukagua maabara hiyo, chumba cha tiba mtandao na kukagua utoaji wa huduma katika taasisi hiyo.

Maabara hiyo ya kisasa imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 7.9 ambazo zimetolewa na Serikali ya awamu ya Tano ikihusisha ununuzi wa mtambo kutoka Kampuni ya Simens ya Ujerumani.

Baada ya kukagua huduma mbalimbali taasisi hiyo, Dkt Ndungulile amewaagiza wataalamu kukamilisha haraka maabara hiyo na chumba cha kutoa huduma ya tiba mtandao ili huduma ianze kupatikana Juni, mwaka huu.

“Natoa maelekezo kwamba ujenzi na usimikaji mitambo ukamilike na ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni, mgonjwa wa kwanza awe ameshahudumiwa hapa,” alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndungulile amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa huduma tiba mtandao, wataalamu wa MOI na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) watatumika kutoa huduma kwa hospitali za mikoa na wilaya.

“Wagonjwa watakaopigwa picha za X- ray katika hospitali za mikoa au wilaya zitatumwa katika chumba cha tiba mtandao na kusomwa na wataalamu wa Muhimbili na Moi na kisha kutumwa mikoani na wagonjwa kupatiwa majibu yao,” amesema Dkt. Ndugulile.

Pia, Dkt. Ndugulile amewataka watumishi wa afya nchini kuendelea kupokea wagonjwa wanaokabiliwa na magonjwa ya msingi sambamba na kupatiwa huduma ya maambukizi ya Covidi-19 endapo watakuwa wameambukizwa.

“Watumishi wenzagu wa afya nawaomba msiwanyanyapae wagonjwa, wapatieni huduma hasa wenye magonjwa mbalimbali,” amesema Dkt. Ndungulile.

Naibu Waziri ameataka pia wataalamu wa afya kujilinda katika sehemu za kazi dhidi ya maambuikizi ya Covid-19 kwa kuwa kipaumbele cha Serikali ni kuwalinda watumishi wa afya ili waweze kuwahuduma wagonjwa.

Pia, Dkt. Ndungulile ameipongeza MNH kwa kushona vazi la PPE kwa ajili ya wataalamu wa afya wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona pamoja na MOI ambayo imetengezea kifaa maalum cha kujinginga uso (Face Shield) kwaajili ya kijikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19.