Home Mchanganyiko KAMPUNI YA TDL YAJITOSA MAPAMBANO YA CORONA

KAMPUNI YA TDL YAJITOSA MAPAMBANO YA CORONA

0

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Dk.Gwamaka Mwabulambo (Kulia) akipokea msaada wa lita 250 za  vitakasa mikono kutoka kwa meneja wa kiwanda cha Tanzania Distilleries Ltd (TDL),Aranyaeli Ayo (katikati)  vilivyotolewa na kampuni hiyo kuunga mkono jitihada za serikali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa ajii ya vituo vya afya wilayani humo  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam j,kushoto ni Meneja Mawasiliano wa TBL Plc,Amanda Walter

……………………………………………………………………………..

 Katika jitihada za kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kukabiliana na maambukizi ua virusi vya COVID-19 nchini, Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL) maarufu kama Konyagi, chini ya kampuni mama ya TBL Plc , imetoa msaada wa lita 250 za vitakasa mikono kwa ajili ya matumizi kwenye vituo vya afya wilayani Temeke.

Tangu kuwepo taarifa za kuwepo ugonjwa wa Corona nchini mapema mwezi mmoja uliopita, kumekuwepo na mahitaji makubwa ya vitakasa mikono kwa ajili ya kujikinga, kwenye makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo vituo vya afya ambapo makampuni na wadau mbalimbali wanaendelea kujitoa kusaidia changamoto hiyo.

Meneja wa kiwanda cha TDL, Aranyaeli Ayo ,amesema wakati wa hafla ya kukabidhi vitakasa mkono kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Temeke, kuwa kampuni kama mdau wa kuzalisha vinywaji vikali ambavyo moja ya malighafi zake zinatumika kutengeneza vitakasa mikono vyenye ubora imejitoa katika kipindi hiki kuhakikisha inaunga mkono jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa Corona kwa kuto msaada wa bidhaa hizo.

Aliongeza kusema kuwa kampuni inaamini kuwa kuwepo kwa jamii yenye afya njema na mazingira tulivu ni muhimu kwa taifa.  Alishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya kupambana na ugonjwa wa Corona na kuongeza “Tutaendelea kujitoa katika kukabiliana na janga hili kama ambavyo leo tumetoa vitakasa mikono kwa ajili ya kutumika katika vituo vya afya na tunaamini tukishirikiana pamoja tutashinda vita hii” alisema Ayo.

 Akipokea msaada huo, Mganga Mkuu wa wilaya ya Temeke, Dk.Gwamaka Mwabulambo, aliishukuru kampuni hiyo kwa kusaidia vituo vya afya wilayani humo na kuwataka wadau wengine kuendelea kujitokeza kuunga mkono jitihada za serikali kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa wa Corona nchini.