Home Mchanganyiko NEC WILAYA YA WETE IMEFUATA MAELEKEZO YANAYOOLEWA NA SERIKALI KUJIKINGA NA CORONA...

NEC WILAYA YA WETE IMEFUATA MAELEKEZO YANAYOOLEWA NA SERIKALI KUJIKINGA NA CORONA KWENYE VITUO VYA KUJIANDIKISHA

0

******************************

Na Masanja Mabula ,PEMBA.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi –NEC- Wilaya ya Wete imesema imefuata maelekezo yote yanayotolewa na Serikali kwa kuweka vifaa vya kinga dhidi ya virusi vya Corona kwenye vituo vyote vya kujiandikisha.

Pamoja na maandalizi hayo lakini ni wananchi wachache sana waliojitokeza kujiandikisha ambapo baadhi ya wananchi walisema hofu ni kupata maambukizi ya virusi vya Corona.

“Tunatakiwa kuepuka mikusanyiko ya watu, hivyo mimi ninahofu kuhusu usalama wa maisha yangu , nasubiri siku ya mwisho nitaendela kwani nahisi watu watakuwa wamepungua”alisema Mariam Said.

Baadhi ya maafisa wasaidizi uwandikishaji walisema vituo vyote vilivyopangwa na tume kwa ajili ya uwandikishaji vimeandaliwa kulinda usalama wananchi wanaokwenda kujiandikisha.

Juma Massoud Juma Afisa Msaidizi kituo  Cha skuli ya Bopwe aliwatoa hofu wananchi kwamba tahadhari zinazoelezwa na wataalamu wa afya zimezingatiwa kwenye kituo hicho.

“Tumeweka ndoo ,sabuni pamoja na vitakasa mikono, hivyo ni lazima kila mwananchi anawe mikono kwa maji tiririka lengo ni kuwakinga na virusi vya Corona”alifahamisha.

Salim Shaib Kaimu Afisa Msaidizi Kituo cha Skuli  ya Mitiulaya bado mwitikio wa wananchi ni mdogo kwa ajili ya kuandikisha kutokana na changamoto ya mvua.

“Hali ya hewa nahisi imechaagia wananchi kutojitokeza kama ambavyo tulitarajia”alieleza.

Licha ya zoezi hilo kwenda kwa mwendo wa kusuasua lakini mawakala wa vyama vya siasa wanapongeza ushirikiano wanaoupata kutoka Tume ya chaguzi-NEC-.

Mohammed Omar.wakala chama cha Demokrasia na maendeleo –CHADEMA-,na Mohammed Ali Saidi wakala wa Chama Cha Mapinduzi – CCM-, walisema wanaimani kwamba siku ya mwisho idadi ya wananchi wanaokwenda kujiandikisha itaongezeka.

“Leo kweli wananchi kidogo sana waliojitokeza , lakini nina imani kwamba siku zijazo idadi itaongezeka”alisema Mohammed Ai Said.

Kwa upande  wao Juma Omar Kombo wakala wa chama cha ACT wazalendo na Zuwena Ali wakala wa Chama cha  ADC, walisema kutokana na maadalizi yaliyofanywa na Tume hakuna mwananchi aliyetiza sifa ambaye ameshindwa kujiandikisha.

Afisa uwandikishaji  tume ya taifa ya uchaguzi –NEC- wilaya hiyo  Issa Juma Hamad alitaja sababu zinazosababisha kudhorota kwa zoezi hilo ni kutokana na ugonjwa COVID-19 na mvua zinazoendelea kunyesha.

Hata hivyo aliwataka wananchi wote waliotimiza sifa kuitumia fursa hiyo kujiandikisha ili waweze kupata nafasi ya kumchugua kongozi wanaye mtaka.

“Bila ya kujiandikisha huwezi kupiga kura, hivyo itakuwa umekoasa haki yako ya msingi ya kuchagua viongozi ktika uchaguzi mkuu hapo baadaye”alisisitiza.

Mkuu wa Wilaya ya Wete Kepteni Khatib Khamis Mwadini amefanya ziara ya kutembelea vituo na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha.