Home Mchanganyiko WAZIRI HASUNGA AZINDUA BODI MPYA NA KUSHAURI NFRA KUJIENDESHA KWA FAIDA

WAZIRI HASUNGA AZINDUA BODI MPYA NA KUSHAURI NFRA KUJIENDESHA KWA FAIDA

0

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akitoa hotuba yake wakati wa tukio la uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo Makao Makuu Jijini Dodoma

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Yustak Kangolle leo kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo, Makao Makuu, Jijini Dodoma

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bwana Milton Lupa akitoa hotuba ya
kuhitimisha hafla ya tukio la uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo, Makao Makuu, Jijini Dodoma

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiwa Mwenyekiti na
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo, Makao Makuu, Jijini Dodoma.

********************************

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (leo) tarehe 28 Aprili, 2020 ameizindua Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na kutoa maelekezo kwa Taasisi hiyo kutoa huduma kwa Watanzania lakini pia kujiendesha kwa faida.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Waziri Hasunga amesema hii ni Bodi ya nne tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo mwaka 2007.

Waziri Hasunga amesema Bodi hiyo pia inawajibu wa kumshauri kwenye mambo ya muhimu na ya msingi, likiwemo masuala la Sera na Miongozo kwenye ununuzi, uhifadhi wa chakula kimkakati.

“Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Wajumbe wa Bodi; Thamani iliyo mbele yenu ni kubwana naomba mtimize pia jukumu la kuisimamia Menejimenti ya NFRA ili kuhakikisha
kuwa, inajiendesha kibiashara bila ya kusahau wajibu wa kutoa huduma kwa umma”.

“Tunashukuru Mradi mkubwa wa ujenzi wa vihenge vya kisasa “Silos” unaendelea vizuri, na tuna uhakika baada ya kukamilika, akiba yetu itafika tani 501,000, nataka mwaka huu mnunue chakula, kuanzia tani 120,000.”Amekaririwa Waziri Hasunga.

Waziri wa Kilimo amesema; kuna fursa ya kuuza chakula nje ya nchi na kuongeza kuwa, NFRA inapaswa kutafuta masoko kwa nguvu zote, ndani na nje ya nchi.

Waziri Hasunga ameipongeza NFRA kwa kuanzisha Kitengo cha Masoko ya Kimkakati na kusistiza kuwa, soko lipo kwenye nchi jirani na kwa kuzingatia kuwa msimu huu wa
kilimo ni Tanzania pekee ndiyo hakushambuliwa na nzige wekundu, lakini Kenya, Uganda na maeneo mengine yalipata changamoto hiyo.

“Tafuteni masoko ndani na nje ya nchi; Lakini nawahakikishia soko lipo nchini Kenya, Uganda, Zimbabwe, Sudan Kusini, Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo”.

Waziri Hasunga ametoa angalizo kuwa baada ya NFRA kupata masoko, Menejimenti inapaswa kuingia mikataba ya kuuza chakula kwa faida na maslai mapana ya Taifa ni si bora kuuza tu.

“Ingieni mikataba yenye tija kwa maslai mapana ya Taifa lakini kwa kulitekeleza jambo hilo kiufanisi, zitumie Balozi zetu zilizopo nchi za jirani, wao wana nafasi nzuri ya kutupa picha nzuri ya masoko na nani wa kufanya naye biashara”. Amemalizia Waziri Hasunga.

Naye Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri ya NFRA, Mhandisi Yustak Kangolle amesema, maagizo, maelekezo na ushauri wa Waziri wa Kilimo una mambo mengi ya
msingi na yeye hana budi kuufuata na kuuzingatia.

“Huu ni muda wa kufanya kazi na napenda kumshukuru Waziri wa Kilimo kwa kuwa na imani nami pamoja na Wajumbe wengine wa Bodi; tunaahidi kufanya kazi kwa
kuzingatia misingi ya taratibu za uendeshaji wa Bodi hii”. Amekaririwa Mhandisi Kangolle.