Home Mchanganyiko NAIBU MEYA WA MANISPAA YA MOROGORO AZIKWA NA WATU 10

NAIBU MEYA WA MANISPAA YA MOROGORO AZIKWA NA WATU 10

0

*********************************

NA FARIDA SAIDY,MOROGORO

Katika kuepusha mikusanyiko isiyoyalazima Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe Isiyaka Sengo amezikwa April 28, 2020 katika makaburi ya kola mkoani Morogoro na mazishi yake kuhudhuriwa na watu kumi na kugharamiwa na serikali.

 

Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa morogoro Mhe Loata Sanare,wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hichi cha vita dhidi ya virus vya corona na kuepuka mikusanyiko.

 

Katika hatua nyingine Mhe Sanare ameendele kuwasisitiza wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya sambamba na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na uvaaji wa barakoa katika maeneo yenye misongamano ikiwemo sokoni na kwenye vyombo vya usafiri wa umma.