Home Mchanganyiko JUMUIYA YA MABOHORA TANZANIA WAMKABIDHI RC MAKONDA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA.

JUMUIYA YA MABOHORA TANZANIA WAMKABIDHI RC MAKONDA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA.

0

****************************

Na Magreth Mbinga.

Jumuiya ya Dawoodi Bohora Tanzania leo imekabidhi vifaa mbalimbali vya kujikinga na corona vyenye thamani ya Shilingi Milioni 27 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa lengo la kuwakinga wananchi wa Mkoa huo.

Amezungumza hayo Mwakilishi wa Mabohara Bw.Murtaza Adanije wakati akikabidhi msaada wa vifaa vya kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona vyenye thamani ya shilingi millioni 27 jijini Dar es salaam.

Pia amesema watu wote wanapaswa kuungwa mkono katika mapambanao dhidi ya ugonjwa huu ili waweze kupambana na Virusi hivyo.

Vilevile mganga mkuu wa Mkoa Rashidi Mfaume amewashukuru wadau ambao wanaendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na Corona kwa kuendelea kutoa misaada mbalimbali.

Sanjari na hayo Bw.Mfaume amesema wao kama sekta ya afya wataendelea kufanya kazi bila kurudi nyuma na Jumuiya ya mabohara hawajaanza hawajaanza leo kutoka misaada kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huu toka uingie hapa nchini.

Hata hivyo amewataka wananchi waendelee kufata maelekezo yanayotolewa na wizarabya afya kupitia vyombo vya habari itasaidia katika kupambana na ugonjwa huu.