Home Mchanganyiko FAMILIA YA KIMBAU YAOMBOLEZA MSIBA WA ABDULKARIM SHAH BUJJI

FAMILIA YA KIMBAU YAOMBOLEZA MSIBA WA ABDULKARIM SHAH BUJJI

0
Familia ya aliyekuwa mbunge wa Mafia marehemu Kanali mstaafu Ayoub Kimbau tumepokea msiba wa ndugu yetu kaka yetu jamaa yetu mbunge mstaafu wa Mafia Ndg. Abdulkarim IH Shah (Bujji) kwa mshtuko na masikitiko Makubwa sana…
Marehemu Shah (Bujji) pamoja na tofauti zetu za kisiasa baina yake na familia yetu hususan katika wakati wote wa zile kampeni za kisiasa, bado alikuwa ni mtu mwenye upendo nidhamu  utu heshima na uungwana wa hali ya juu hasa kwa wazazi wetu na sisi watoto.Buji alikuwa kaka, rafiki, mtani na kiongozi wetu mstaafu tutamkumbuka siku zote..
Mungu awatie nguvu na awape moyo wa subra ndugu na jamaa na watoto wake wote katika kipindi hiki kigumu…kipekee tunampa pole sana mke wa marehemu Bi. Naila kwa kumpoteza mwenza na baba wa watoto wake..
Mungu awape moyo wa subra na aweke roho ya marehemu kaka yangu rafiki yangu Bujji mahala pema peponi
 
ILWIR🙏
Omary Ayoub Kimbau
(Kwa niaba ya familia ya Kimbau)