Home Mchanganyiko RC SINGIDA ATOA FUTARI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN KWA WAISLAMU

RC SINGIDA ATOA FUTARI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN KWA WAISLAMU

0
 Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mbwana Mtingule (kulia) akimkabidhi viazi vitamu Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Alhaj  Burhan Mlau vilivyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi kwa ajili ya futari ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu wa mkoa huo leo.
Viazi vya futari vikishushwa kwenye gari.

Viazi vya futari vikiingizwa ndani ya stoo ya ofisi ya Bakwata Mkoa wa Singida.

Viazi vya futari vikiingizwa ndani ya stoo ya ofisi ya Bakwata Mkoa wa Singida.

Shehena ya viazi vilivyo tolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi.
Ofisi ya Bakwata Mkoa wa Singida.Boniphace Jilili na Dotto Mwaibale, Singida.

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa chakula kwa waumini wakiislamu Mkoa huo  kama sehemu ya futari katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Akikabidhi msaada huo wa Viazi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa katibu wa Mkuu wa Mkoa Mbwana Mtingule alisema Dkt. Nchimbi ametoa chakula kwa makundi yasiyojiweza ndani ya waumini wa Kiislamu Mkoa huo ili waweze kufuturu na kufanya ibada yao kuwa kamili

Alisema Mkuu wa Mkoa amewaomba waumini hao kuendelea kumuomba mwenyezi Mungu katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan ili atuepushe na mambo mabaya yanayotokea hapa nchini ikiwemo magonjwa.

Aidha wakati akipokea msaada huo wa viazi Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida,  Alhaj Burhan Mlau alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwajali Waislamu kwani kila Mwaka anakuwa wa kwanza kutoa futari kwa waumini hao.

“Nimpongeze Mama yetu Mkuu wa Mkoa kila Mwaka haachi kutoa futari kwa waislamu tena Mwanzoni kabisa mwa mwezi, Mwaka jana alitoa Mchele na Sukari, Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda na kumpa moyo huo huo.”alisema Mlau

Alhaj Mlau alisema atahakikisha futari hiyo inawafikia walengwa ambao ni wazee wasiojiweza, wajane na yatima ili kwa siku hizo chache waweze kufuturu na kupunguza makali ya mfungo


Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka waumini hao kuachana mita moja wanapokuwa wakiswali na kuhakikisha wanapuliza dawa kwenye Msikiti Mara baada ya swala ili kutii maagizo ya Wizara ya afya yatakayopelekea kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Corona