Home Mchanganyiko Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Tahadhari Dhidi ya...

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Tahadhari Dhidi ya Kusambaa kwa Virusi vya Corona

0

………………………………………………………………………………….

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kuzingatia tamko la Serikali kuhusu tahadhari ya kusambaa kwa ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, inatoa mwongozo ufuatao, unaopaswa kuzingatiwa na wananchi wote wanaofika katika ofisi za Tume kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali:-

  1. Wananchi wote wanaotarajia kufika ofisi za Tume kwa ajili ya kuwasilisha na kufuatilia malalamiko yao, ama kwa shida nyingine za ki-ofisi na binafsi wawe wamevaa barakoa.

  1. Wananchi walio na malalamiko yanayohusisha kikundi cha watu, wateuwe wawakilishi wasiozidi wawili (2) watakaofika Tume kuwawakilisha badala ya kufika kwa kikundi.

  1. Aidha, katika kipindi hiki Wananchi wanahimizwa kutumia zaidi utaratibu wa kuwasilisha malalamiko bila kufika ofisi za Tume kwa kutumia njia ya barua, ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani (SMS), simu na barua pepe (e-mail) kwa kutumia anuani na namba za simu zilizopo hapa chini.

Mawasiliano yote yaelekezwe kwa Mwenyekiti, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kwa kutegemeana na mahali ulipo, tuma barua yako kwa kutumia moja ya anuani zifuatazo:

S.L.P. 1049, DODOMA; Simu: 0734 047 775/0734 119 978; Barua pepe: [email protected] au 

S.L.P. 285, ZANZIBAR; Simu: (024) 2230494/236124 au 

S.L.P. 2643, 11101 DAR ES SALAAM; Simu: (022) 2135747/8; Barua pepe: [email protected] au  

S.L.P. 10430, MWANZA; Simu: (028) 2541770; Faksi (028) 2541770 au 

S.L.P. 1050, LINDI; Simu: (023) 2202734/2202744 au

S.L.P. 231, WETE – PEMBA; Simu: (024) 2454196.

Kuwasilisha lalamiko kwa njia ya ujumbe mfupi

Tuma ujumbe wa simu ya kiganjani (SMS) kwenda Na. 0737 446 787, ukianzia na neno ‘REPORT’. Mfano: REPORT Shule ya Msingi Kinondoni, DSM tunachapwa viboko zaidi ya 10.

Kufuatilia lalamiko lililokwisha wasilishwa

Tuma ujumbe wako ukianza na neno ‘STATUS’ kwenda Na. 0737 446 787. Mfano: STATUS 13024 (13024 ni mfano wa namba ya lalamiko atakayokuwa amepewa Mlalamikaji).

Kwa maelezo zaidi piga simu Na. 0734 047 775/0734 119 978 au tuma barua pepe kwenda: [email protected] 

MUHIMU: Mlalamikaji aandike jina, anwani yake, namba ya simu na anuani ya barua pepe (kama anazo) ili Tume iweze kuendeleza mawasiliano. 

Ni matumaini ya Tume kuwa wananchi watazingatia mwongozo huu ili kuendelea kufurahia huduma kutoka Tume katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya gonjwa hatari linalosababishwa na virusi vya Corona.