Home Burudani MBUNGE CHUMI ASHAURI COSOTA IFANYIWE MAREKEBISHO KUINUA TASNIA YA FILAMU NCHINI

MBUNGE CHUMI ASHAURI COSOTA IFANYIWE MAREKEBISHO KUINUA TASNIA YA FILAMU NCHINI

0
…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi  (CCM)amesema kuwa urasimu na Mlolongo mrefu katika kupata huduma kwenye ofisi za COSOTA unakwaza wasanii na kudhoofisha tasnia ya Filamu. 
Akichangia wakati wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Chumi amesema kuwa tasnia ya sanaa, habari na burudani ( media and entertainment industry)  ina mchango mkubwa katika kuingiza mapato ya serikali hata hivyo Mlolongo na mtawanyiko kwenye Vyombo kama Cosota, Bodi ya Filamu na Basata vinafifisha jitihada za Vijana katika kujiajiri na kuliongezea Taifa mapato. 
Akizungumza kwa takwimu, mbunge huyo amesema kuwa kwa mujibu wa Taarifa ya PWC “Entertainment and Media Outlook 2018-2020” kutakuwa na ongezeko kubwa la mapato  katika nchi za kiafrika na duniani kwa ujumla Kati ya mwaka 2017 mpaka 2022.
Ametolea mfano wa baadhi ya nchi ambapo  Kenya mapato yataongezeka kutoka dola za marekani Bil. 1.7 mpaka Bil. 2.9 kufikia mwaka 2022, Tanzania kutoka milioni 496 mwaka 2017 mpaka Bil.1.1 mwaka 2022, Ghana kutoka milioni 752 mpaka Bil .1.5, Nigeria kutoka Bil 3.8 mpaka Bil 9.9
Ameogeza kuwa kwa upande wa Filamu mapato Kati ya 2017 na 2022 yataongezeka kwa Kenya kwa dola za kimarekani kutoka Mil 4.5 mpaka Mil 5.9 Tanzania kutoka 710,000 mpaka Mil 1.5, Ghana kutoka Mil1.6 mpaka  Mil 2.1, Nigeria kutoka Mil 12 mpaka Mil 18 dola za kimarekani. 
Mbunge huyo amesema, tasnia hii inapaswa kutengenezewa mazingira bora kwa kuwa inaingiza mapato lakini pia inaajiri maelfu ya Vijana. 
“Niliwahi kushauri kuwa Kama sio kila mkoa basi tuanze na Kanda, kuliko ilivyo sasa msanii lazima uende Cosota Dar, afu aende Bodi ya Filamu afu aende Basata, Kwanini huduma hizi zisiwe sehemu mmoja au muwatumie maafisa Utamaduni katika Wilaya” amesema Chumi.
Akizungumzia michezo, Chumi ameitaka serikali kuona uwezekano wa kuwa na shule maalum za vipaji vya michezo na Utamaduni Kama ilivyo kwa shule za vipaji za taaluma.
Aidha ameishauri TFF kuliangalia kwa ukaribu suala la malipo ya waamuzi ili waweze kuchezesha kwa haki, na ikibidi kutafuta mdhamini ambaye atashughulikia kulipa posho za waamuzi tu.
“Ili kuvutia wadhamini, lazima pawepo na ushindani, lakini pia uwazi na uwajibikaji” amesema.
Amesisitiza mbunge huyo ambaye pia ni mwanamichezo.