Home Mchanganyiko ZOEZI LA UWEKAJI MIPAKA ENEO LA CHAMANANGWE LIMELENGA KUDHIBITI UVAMIZI ENEO HILO

ZOEZI LA UWEKAJI MIPAKA ENEO LA CHAMANANGWE LIMELENGA KUDHIBITI UVAMIZI ENEO HILO

0

…………………………………………………………..

Na Masanja Mabula ,PEMBA      

SERIKALI ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imesema zoezi la uwekaji wa mipaka ya  eneo la Chamanangwe lililotengwa kwa ajili   ya ujenzi wa viwanda limelenga kudhibiti uvamizi katika eneo hilo.

Aidha zoezi hilo pia litawezesha kuwatambua wananchi wenye vipando vyao na hiyo kurhisisha ulipaji wa fidia ya mazao yao.

Akizungumza baada ya kulitembelea zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba  Omar Khamis Othman alisema serikali haiwezi kumdhulumu mwananchi mwenye vipando katika eneo hilo na kwamba kila mmoja atapata haki yake.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema licha ya serikali kuanza kulipa fidia , kuna baadhi ya wananchi wameshindwa kujitokeza jambo ambalo linakwamisha shughuli za ujenzi wa viwandaa katika eneo hilo.

“Tumchoka kuwabembeleza, tunakusudia kuweka mipaka na wale ambao vipando na mazao yao yatakuwa katikati ya mioaka wanatakiwa kufika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Wete kuchukua fidia zao”alifahamisha.

Afisa mdhamini wizara ya ardhi,nyumba na nishati Pemba Juma Bakar Alawi aliwataka wananchi wenye vipando kujitokeza kuchukua fidia zao.

Alisema ni vyema wananchi watafahamu kwamba ardhi ni mali ya serikali , hivyo kusita kwenda kuchukua fidia haiwezi kuizuia serikali kulichukua eneo hilo na kulitumia kwa shughuli za viwanda.

“Hata kama hawatakuja kuchukua fidia zao, sio sababu ambayo itaizuia serikali kuitumia ardhi kwa shughuli za maendeleo kwani ardhi ni mali ya serikali”alieleza.

Kwa upande wake Afisa Mdhamin Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Pemba Ali Suleiman  aliisema eneo lote limeshafayiwa tathmini  na baadhi ya wananchi wameshalipwa fidia.

“Baadhi ya wananchi wenye vipando katika eneo hili walishalipwa fidia zao, na hawa waliobakia fedha zao zipo pindi wakihitaji watapewa”alifahamisha.

Vikosi vya ulinzi na usalama mkoa huo vimetoa tahadhari kwa mwananchi yoyote atakae jaribu kukwamisha zoezi hilo.

“Baada ya serikali kuweka mipaka yake ,tutona nayejaribu kukwamisha zoezi hili , tutamshughulikia ipasavyo”alisema Juma Ngwali Mkuu wa kitengo cha mawasiliano KMKM Pemba.

Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba kaatika kuunga mkono azma ya serikali la kufanya nchi ya viwanda  ,imetenga eneo la Chamanangwe kuwa ni la ujenzi wa viwanda mbali mbali ikiwemo cha Chumvi na Mwani.