Home Michezo BEKI WA SIMBA SC AFIWA NA BABA YAKE MZAZI MKOANI MOROGORO

BEKI WA SIMBA SC AFIWA NA BABA YAKE MZAZI MKOANI MOROGORO

0

BEKI wa kushoto wa klabu ya Simba, Gardiel Michael Mbaga amefiwa na baba yake mzazi, Michael Mbaga Kamagi leo mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu yake, baba yake amefariki mjini eneo la Bwawani mkoani Morogoro na ripoti zinasema alikuwa anaumwa.
“Mchezaji wetu Gardiel Michael amefiwa na baba yake leo asubuhi. Tunatoa pole kwa Gardiel, familia, ndugu, jamaa na marafiki wote kwa kuondokewa na mpendwa wao,”imesema taarifa ya klabu ya Simba leo.

Michael Mbaga Kamagi leo mjini Morogoro.Gardiel yupo katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe Simba SC akitokea kwa mahasimu, Yanga SC alikodumu kwa misimu miwili baada ya kuwasili akitokea Azam FC iliyomuibua katika mfumo wake wa soka ya vijana.