Home Mchanganyiko WATANZANIA TUTAKUFA KWA TABIA YA KUPINGA KILA KITU

WATANZANIA TUTAKUFA KWA TABIA YA KUPINGA KILA KITU

0

……………………………………………………………………………………………….

Yaani imekuwa tabia kila maelekezo yanayotolewa na viongozi kundi la watu fulani wachache mnapinga. Hata hili la Mask au balakoa mmeanza KUPINGA kweli?

Hivi mtaelimika lini ? Someni kwenye tovuti mbalimbali mpate elimu. Soma habari za CDC Marekani, CNN,BBC na WHO, mpate elimu. Msipinge kila kitu. Mnapinga Kwa kuwa kasema RC Makonda au Gavana wa New York Andrew Cuomo
Huwezi kununua Mask za mwezi mmoja tu na familia yako Mask za Surgical 50pc Kwa bei 160,000 mask moja unavaa Kwa masaa manne tu na unatupa, N95 bei ya 95,000
Jiulize swali wewe na familia yako mtanunua ngapi? Baada ya miezi mitatu.
Yaani watu wetu Kwa kujitia ujuaji wanapambana kumpinga RC Makonda uku watu wa jimbo la New York Marekani wanafata maelekezo ya Gavana wao ambayo ayatofautiani kabisa na aliyotoa RC Makonda Kwa Dar es Salaam

Someni hata habari za nje mjifunze na kwa wengine la sivyo utabaki pekeyako

Suala la kujikiga na corona ndugu zangu ni suala binafsi na familia yako. Wanaojali afya zao wanachukua taadhari zinazotolewa.
Waacheni wale wapingaji kule Instagram na tweeter wabebe msalaba wao, waambieni sisi tunachukua hatua, maana yake kama ni kufa unakufa ukiwa peke yako