Home Mchanganyiko MWENENDO WA KESI YA HAMAD NASSOR MKOANI WA KASKAZINI PEMBA

MWENENDO WA KESI YA HAMAD NASSOR MKOANI WA KASKAZINI PEMBA

0

****************************

WAKAAZI wa shehia ya Pandani Wilaya ya Wete wametilia wasiwasi juu ya mwenendo wa mashauri sita ya udhalilishaji yanayomkabili Hamad Nassor Hamad 73 yanayosikilizwa katika mahakama ya mkoa wa Kaskazini Pemba.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi walisema mwenendo wa kesi hizo unawapa mashaka ikizingatiwa kwamba mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana.

Baadhi wa wazazi wa watoto waliodhalilishwa walisema mahakama inaendesha kesi hizo kwa mwendo wa kusuasua kwani zimechukua muda mrefu bila ya kutolewa hukumu.

“Hizi ni kesi za mwaka 2018 hadi leo zinaendelea kupigwa danadana , lakini kuna baadhi ya kesi zinachukua mwezi mmoja kupatiwa hukumu tunashangaa kwa hizi”alisema mmoja  wa wazazi.

Kesi hizo zilipangwa kusikilizwa tarehe 20/04/2020 katika mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba lakini zimelazimika kuahirishwa na hakimu wa mahakama ya Mwanzo Wete na kupangiwa tarehe 31/04/2020.

Hakimu wa mahakama ya Mwanzo Wete Maulid Ali Hamad alilazimika kuahirisha kesi hizo kutokana na hakimu wa mahakama ya Mkoa kutokuwapo mahakamani.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inasema kwamba kosa la kwanza mpaka la tatu yanafanana , ambapo aliyatenda siku na mwezi usiofahamisha mwaka 2018,kwa kuwaruhusu watoto wenye umri wa miaka 9, 8 na 10 kubakia ndani ya nyumba yake kwa ajili ya kushiriki onesho chafu lisilofaa.

Watoto hao walibakia ndani ya nyumba yake na kushiriki uoneshaji wa DVD ya picha za ngono jambo ambalo ni kosa kisheria chini ya kifungu cha 138(1) (a) cha sheria ya adhabu namba 6/2018 sheria ya SMZ.

Kosa la nne ni unyanyasaji mkubwa wa kijinsia alilomfanyia msichana mwenye umri wa miaka 9, chini ya kifungu cha 139(1),(a),(2) na (b) cha sheria ya adhabu namba 6/2018.

Aidha kosa la tano  ni shambulio la aibu sawa na kosa la sita , kinyume na kifungu cha 114(1) cha sheria ya adhabu namba 6/2018 , ambapo watoto wadogo wenye umri wa miaka 8 anadaiwa kuwafanyia kitendo hicho.

Mratibu wa  Chama cha Wandishi wa Habari wanawake TAMWA Pemba Fat-hiya Mussa aliendelea kuishauri jamii kutovunjika moyo bali wajiandae kwenda kutoa ushahidi mahakamani wakati ukifika.