Home Mchanganyiko MUSSA KILAKALA AONGOZA MAPAMBANO YA KUKATA MNYORORO WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA...

MUSSA KILAKALA AONGOZA MAPAMBANO YA KUKATA MNYORORO WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA KORONA DAR ES SALAAM

0

***********************************

Umoja wa Vijana wa CCM (M) Dar es salaam leo wamezindua program maalum ya hamasa ya kukata Mnyororo wa maambukizi ya Corona Mkoa wa Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake Ndg.Mussa Ramadhan Kilakala, katika mkakati huo Ndg. Kilakala alikutana na viongozi wa umoja huo wa wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es salaam na kuwapa dira ya namna ya kuifanya hamasa hiyo kwa weledi huku wakizingatia ushauri wa wataalam wa afya wa kijikinga na maambukizi ya virusi hivyo.

Aidha Katibu wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa CCM (M) Dar es salaam Ndg. Ally Mohammed amesema kuwa Corona ni gonjwa la kisayansi sio gonjwa la kisiasa hivyo Umoja wa Vijana (M) Dar es salaam wameonyesha njia na inapaswa kuigwa na vijana wote nchini bila ya kujali itikadi zao, alisema maambukizi hayo kwa mujibu wa taarifa ya shirika la afya duniani yalitabiriwa kushika kasi zaidi katika bara la Afrika kwa sababu ya aina ya maisha yetu na udhaifu wa huduma zetu za afya hivyo alitahadharisha kuwa ugonjwa huo tutaukomesha kwa kuwa na umakini na nidhamu ya hali ya juu katika kufuata maelekezo ya wataalam wa afya ya kunawa maji kwa sabuni,kutumia vitakasa na kuvaa barakoa kila tunapotoka nje ya majumba yetu.

Operation hiyo iliyozinduliwa leo kwa kugawa vifaa vya kujikinga na Korona kwa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM wa wilaya tano za Mkoa wa Dar es salaam sambamba na kutembelea maeneo ya soko la feri na kugawa vitakasa mikono kwa madereva bajaji na pikipiki sambamba na kugawa tenki kubwa la maji kwa uongozi wa soko hilo.

Zoezi hili ni endelevu na linatoa wito kwa wadau wote kuunga mkono juhudi za serikali za kukata mnyororo wa maambukizi ya virusi vya Corona Tanzania hususan Mkoa wa Dar es salaam ambapo ndio kunaongoza kwa maambukizi mengi.

Uimara wa afya yako ndio uimara wa taifa lako tutashinda Corona,tutavuka salama