Home Mchanganyiko MAKONDA AWASIHI WANANCHI KUVAA BARAKOA KUANZIA JUMATATU, AZIOMBA KAMPUNI ZA SIMU KUWEKA...

MAKONDA AWASIHI WANANCHI KUVAA BARAKOA KUANZIA JUMATATU, AZIOMBA KAMPUNI ZA SIMU KUWEKA “RING TONE” ZA KUELIMISHA WANANCHI KUHUSU CORONA

0

………………………………………………………………..

Na Magreth Mbinga

Makampuni ya simu yatumie ringtone zao kwaajili ya kutoa elimu dhidi ya ugonjwa huu harari wa Corona badala ya kuweka nyimbo za kawaida ili kusaidia kupambana na ugonjwa huu .

Kauli hiyo imetolewa na  Mkuu wa Dar es salaam Mh Paul Makonda wakati wa ukaguzi wa kemikali ipatayo lita laki moja na sabini iliyo kamatwa na mamlaka ya kushibiti na kupambana na madawa ya kulevya.

Makonda amewasihi wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanavaa Barakoa (Mask) kuanzia Jumatatu ya April 20 kila wanapokwenda kwenye maeneo ya Masoko na Vituo vya Daladala ili kujikinga na Janga la Virusi vya Corona.

RC Makonda pia ameelekeza wafanyabiashara wote wa mkoa huo kuhakikisha bidhaa wanazouza zinakaa kwenye vifungashio vya kubeba na kuondoka (Take away) ili kupunguza mikusanyiko.

Naye M kemia mkuu wa serikali Dk Fidelis amesema kiwango kilichopo katika kemikali hiyo kinafaa katika utengenezaji wa vitakasa mikono wataigawa katika viwanda ambavyo vinatengeneza vitakasa mikono hivyo.

Hata hivyo kaimu kamishina jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulenya amesema James Khaji amesema kemikali iliyokamatwa wameikabidhi kwa mkemia mkuu kwaajili ya kutengeneza vitakasa mikono