Home Burudani DUGE MAFIGHTER AACHIA NGOMA “CORONA”

DUGE MAFIGHTER AACHIA NGOMA “CORONA”

0

**************************

NA EMMANUEL MBATILO

Tukiwa katika vita ya kupambana na Maambukizi ya Virusi vya Corona hapa nchini na Duniani Kote kwa Ujumla, Msanii wa kizazi Kipya Duge Mafighter ameamua kuachia kichupa kinachokwenda kwa jina la Corona ili kuendeleza kutia hamasa kwa jamii jinsi gani unaweza kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Duge ameiomba jamii iendelee kufuata utaratibu uliowekwa na wataalamu wa afya namna ya kujikinga na maambukizi hayo ili kuweza kuepuka maambukizi pamoja na kusambaa.

Aidha Duge ameongeza kuwa uwepo wa uelewa mdogo kwa baadhi ya Watanzania wachache unaweza kusababisha maambukizi hayo kusambaa hivyo ameiomba jamii kuendelea kuhamasika na kupokeea elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi hayo.

“Ukiingia kwenye mitaa tumeona vijana wengi wanavyohamasika namna ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona hii yote ni juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Afya kutoa elimu ya kutosha namna ya kujikinga na maambukizi haya”. Alisema Duge Mafighter.