Home Mchanganyiko Letshego  yasaidia vita dhidi ya ugonjwa wa corona

Letshego  yasaidia vita dhidi ya ugonjwa wa corona

0

Mhasibu wa taasisi ya Lesthego Tanzania (Faidika), Julieth Kileo (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 33 kwa waziri wa Afya, Ummy(wa pili kushoto) Mwalimu kwa ajli ya vita dhidi ya ugonjwa wa corona. Wa kwanza kulia ni   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Letshego, Andrew Lyimo na kushoto ni mwanasheria wa taasisi hiyo, Kenedy Lyimo.

Mhasibu wa taasisi ya Lestshego Tanzania (Faidika), Julieth Kileo (kushoto), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Letshego, Andrew Lyimo (katikati) na kushoto ni mwanasheria wa taasisi hiyo, Kenedy Lyimo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kukabidhi msaada wenye thamani ya sh milioni 33 kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa ajli ya kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona.

*****************************

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Taasisi ya Letshego (Faidika) imekabidhi msaada wa sh milioni 33 kwa serikali kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona.

Mbali ya taasisi hiyo, pia taasisi nyingine tisa nazo zilikabidhi msaada wao kwa serikali na kufanya jumla ya Sh Bilioni 3.2 kupatikana kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Letshego ilikabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alipokea kwa niaba ya waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Katika makabidhiano hayo, pia kampuni ya  simu, Vodacom Tanzania ilikabidhi kiasi cha Sh bilioni 2 huku  Yapı Merkezi ikitoa msaada wenye thamani ya Sh milioni 200.

Taasisi nyingine zilikuwa benki ya NBC iliyokabidhi sh milioni 80 , wakati Shirika la Reli Tanzania lilikabidhi Sh Milioni 65 na Rotary Bahari ilikabidhi msaada wenye thamani ya Sh milioni 15.

Kampuni ya Songas Limited nayo ilikabidhi msaada Sh milioni 100 wakati kampuni ya Bima ya Sanlam ilitoa msaada wa Sh milioni 172.5, Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya fedha Tanzania (FSDT) ikikabidhi Sh million 225 na Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri ikiabidhi msaada wa Sh milioni 10.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Letshego (Faidika) Andrew Tarimo alisema kuwa  wameguswa sana na vita dhidi ya kutokomeza ugonjwa wa corona na kuamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kusaidia Watanzania.

Alisema kuwa msaada wao umelenga kuutokomeza ugonjwa huo nchini na kuungana na Watanzania katika vita hiyo.

“Letshego Tanzania inaungana na Watanzania wote katika vita dhidi ya ugonjwa wa corona.  Kwa sasa Taifa lipo katika janga kubwa ambalo linaathiri maendeleo ya nchi na taasisi yao imeamua kuingia mstari wa mbele katika vita hii,” alisema   Tarimo.

Kwa upande wake, Waziri Mwalimu alisema alizishukuru  taasisi hizo kwa msaada huo kwani unalenga kuutokomeza ugonjwa huo hapa nchini.

Waziri Mwalimu pia aliwataka wananchi kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya kutoka kwa waataalam wa afya na msaada huo utapelekwa kwenye mfuko wa mapmabano ya ugonjwa huo ili kusaidia vita dhidi ya maambukizi.