Home Mchanganyiko RC MAKONDA AMEMSHUKURU ROSTAM KWA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA

RC MAKONDA AMEMSHUKURU ROSTAM KWA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA

0

*********************************

Na Magreth Mbinga

Ninakila sababu ya kumshukuru rafiki yetu Rostam Azizi kwa msaada huu wa vitakasa mikono na barakoa kwa wakati huu kila mmoja anahitaji faraja.

Amezungumza hayo leo MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda wakati wa kupokea msaada huo uliotolewa na mfanyabishara huyo.

Pia Makonda amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kwa kutoa msaada wa magari zaidi ya 25 ambayo yatasaidia kubeba wagonjwa katika vituo ishirini na tano ambavyo vimetengwa zikiwemo hospitali.

“Vifaa vinakuja kwaajili yenu ili viweze kufanya kazi inayotakiwa na sio mukatumie na familia zenu na wale wezi tafadhali musiibe vifaa hivi ni kwaajili ya usalama wenu” amesema Makonda.

Vilevile amesema vifaa hivyo vitasambazwa kwenye daladala ili abiria waweze kujitakasa kabla ya kupanda ndani ya usafiri huo na wananchi wasiwe wabishi .

Sanjari na hayo mfanyabiashara Rostam Azizi amesema Corona ipo Tanzania na Duniani kote na haunatiba ya kutibu ugonjwa huo tiba pekee ni hadhari usiupate.

“Nawaomba wafanyabiashara wenzangu tuweze kusaidia serikali katika kupambana na ugonjwa huu hatari hata nchi za magharibi wafanyabiashara wanasaidiana na serikali kupambana na ugonjwa huu” amesema Rostam.

Hatahivyo Mganga kuu wa Mkoa Rashidi Mfaume amesema MKUU wa Mkoa muda mwangi alikuwa akiwashauri na kuwatia moyo na wadau wengine waendelee kuwaunga mkono na amewasihi wananchi kuwa Corona ipo na inaua wafate maelekezo ya wataalamu wa afya.

Na Rais wa madaktari Elisha Osati amesema anamshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na ugonjwa huo na kuwataka wananchi watumie barakoa wanapoenda hospitali