Home Mchanganyiko DC Chonjo amjia juu mkandarasi wa soko la kisasa Morogoro.

DC Chonjo amjia juu mkandarasi wa soko la kisasa Morogoro.

0

 

****************************

Na Farida Saidy,MOROGORO

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amemtaka Mkandarasi wa Soko Kuu la Kisasa kufanyakazi kwa ushirikiano ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

Hayo ameyasema leo, Aprili 16, 2020 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikiwemo mradi wa Soko pamoja na Stendi ya Daladala.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema mradi huo umekaa muda mrefu sana , hivyo mkandarasi lazima aonyeshe ushirikiano na moyo wa kizalendo katika kutumia fedha za kodi za Wananchi ambazo Mhe. Rais, Dtk. John Magufuli amezitafuta kwa tabu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.

Aidha, amemtaka  Mkandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa,, kuwa mzalendo na kukamilisha mradi huo kwa wakati.

”Muwe wazalendo, mlituambia kwamba mtatuwekea Paa la Soko kwa gharama nafuu, cha ajabu kwamba mkatuambia Bilioni 1.2 , sasa tumeamua kutafuta mzawa mwenye mapenzi mema akatupunguzia hadi kufikia Milioni 859 na VAT juu, nyie  mnawakatalia kuingia Sokoni na kutowapa ushirikiano, ni kitu cha ajabu sana mkiambiwa nyie ndio mnaokwamisha mradi tutakuwa tunawaonea? Mhe. Waziri Jaffo akisikia hii unafikiri itakuwaje? Tuwe wazalendo mradi huu ni wa wananchi , kule tumewapanga kwa muda tunatarajia mradi huu ukamilike ili tuwarudishe hapa na nyinyi mnatukwamisha, shirikianeni mkifanya kazi nzuri ndio mnazidi kujitangaza” Ameongeza DC Chonjo.

Amesema katika ziara ya Mkuu wa Mkoa , walikubaliana kuangalia kiasi nafuu cha kuweka paa la Soko lakini cha kushangaza bei  waliyokuja nayo ni kubwa huku akijua kwamba Manispaa hiyo haina uwezo wa kununua.

”Muwe wazalendo, mlituambia kwamba mtatufanyia kwa gharama nafuu, cha ajabu kwamba mkatuambia Bilioni 1.2 , sasa tumeamua kutafuta mzawa mwenye mapenzi mema akatupunguzia hadi kufikia Milioni 859 nna VAT juu mnawakatalia kuingia Sokoni na kutowapa ushirikiano, ni kitu cha ajabu sana mkiambiwa nyie ndio mnaokwamisha mradi tutakuwa tunawaonea? Mhe. Waziri Jaffo akisikia hii unafikiri itakuwaje? Tuwe wazalendo mradi huu ni wa wananchi , kule tumewapanga kwa muda tunatarajia mradi huu ukamilike ili tuwarudishe hapa na nyinyi mnatukwamisha, shirikianeni mkifanya kazi nzuri ndio mnazidi kujitangaza” Amesema DC Chonjo.

“Ujenzi huu wa mradi wa Soko ulipaswa kumalizika  tarehe 31, Desemba, 2019 lakini kutokana na ukiritimba wake mradi ukachelewa , alishatuambia hawezi kuweka paa kwa bei ndogo, tukatafuta mtu ambaye ataendana na bei zetu tukampata lakini bado akaendelea kumuwekea vikwazo  badala ya kushirikiana na wenzake, kwa maana hiyo inaonekana kuwa  yeye ndio  kikwazo cha kukwamisha mradi huu, katika vikao vyote vya mchakato wa kumpata mtu wa bei nafuu wa kuezeka paa la Soko alishirikishwa leo anakuja kutukwamisha hatuwezi kuvumilia , tunachokiomba waendelee kushirikiana ili mradi huu umalizike kwa wakati”Ameongeza Chonjo.

Amesema Wafanyabiashara wametengewa maeneo kwa muda, lakini wanapokwenda kuwaambia wasipange biashara chini wanaleta chuki na Serikali yao , hivyo lazima Soko hilo likamilike kwa wakati na kuwaondolea adha wafanyabiashara.

Hata hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema Manispaa ya Morogoro imekuwa wazalendo sana kwani imemvumilia  sana Mkandarasi hivyo wao wanatakiwa kuheshimu maamuzi yao kwa kufanya kazi na kukamilisha mradi kwa wakati.

Amesema miradi hiyo inasubiriwa na Wananchi , kwahiyo kukamilika kwa miradi ita pelekea kuanza kutoa huduma bora kwa Wananchi na kuongeza mapato kwa Halmashauri.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim, amesema wameyapokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya hivyo watajitahidi kukaa na Wakandarasi kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.

Naye Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu, amesema mradi wote wa Stendi ya Daladala  umefikia  asilimia 90, ambapo  Jengo la Utawala ni asilimia 95 na Jengo la Ulinzi asilimia 92% hivyo hadi kufikia tarehe 25, mwezi Mei, 2020 mradi huo utakuwa umekamilika licha ya kuwepo kwa changamoto kama vile mvua na uwepo wa ugonjwa wa CORONA.