Home Mchanganyiko JESHI LA UHAMIAJI LAIMARISHA UKAGUZI KWENYE VIZUIZI NJOMBE

JESHI LA UHAMIAJI LAIMARISHA UKAGUZI KWENYE VIZUIZI NJOMBE

0

……………………………………………………………………………

Joctan Agustino,NJOMBE

Jeshi la uhamiaji mkoa wa Njombe limeimarisha ulinzi wa masaa 24 na kuendesha operesheni ya ukaguzi mkali wa magari ya mizigo na abiria katika vizuizi vya barabara kuu za mkoa huo kikiwemo cha Mjini Makambako kinachopitiwa na barabara ya TANZAMU(Tanzania na Zambia) na kubaini idadi kubwa ya madereva hawazingatii miongozo ya wizara ya afya katika kujikinga na mlipuko wa ugonjwa tishio wa CORONA.

Ukaguzi huo ambao umefanyika usiku wa kuamkia april 15 ukiambatana na utoajiwa wa elimu kwa watumia barabara hususani watembea kwa miguu,abiria na madereva umekuwa na mapokeo chanya kwa wananchi ambao wamekuwa hawana elimu ya kina kuhusu namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo.

Awali Kamanda wa uhamiaji mkoa wa Njombe John Yindi na Sajenti Godfrey Mchwekezi wakitoa elimu kwa abiria na madereva mara baada ya kufanya ukaguzi wametaka watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanadai vitu vya kujikinga kabla  ya kuingia kwenye chombo cha usafiri na kisha kuweka bayana kwamba zoezi hilo kutokuwa na kikomo.

Operesheni hiyo inapata mapokeo chanya kwa madereva akiwemo Nikson Salingo ambao wanasema itasaidia kudhibiti maambukizi mapya na kueleza jitihada wanazochukua kujikinga pamoja na athari wanazokutana nazo katika kipindi hiki cha mlipuko.

Mbali na kutoa elimu ya corona jeshi hilo pia limekagua vitamburisho vya urai yanayotoka nje ya nchi katika barabara ya TANZAMU inayounganisha nchi ya Tanzana na Zambia ambayo imekuwa na mikasa mingi ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyemela.