Home Mchanganyiko MAVUNDE SINA PRESHA NA WANADODOMA IFIKAPO OKTOBA 2020

MAVUNDE SINA PRESHA NA WANADODOMA IFIKAPO OKTOBA 2020

0
…………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde amesema kuwa hanapresha na Uchaguzi wa Oktoba Mwaka huu kulingana na kutekeleza aliyoyaahidi na waliyoyataka waajiri wake ambao ni wananchi wa Jimbo hilo.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa kituo hiki lililohoji kuwa Jimbo la Dodoma Mjini halijawahi kuongwozwa na mtu mmoja kwa awamu mbili?
Mavunde amesema kuwa yeye hanawasi wasi na wananchi wake kwani wao ni mashahidi wameweza kuona awali jimbo lilikuwaje na leo liko wapi katika maendeleo.
“Hivyo muda wa kufanya hukumu juu yangu ukifika wananchi wangu watafanya tathimini na kuhamua nani apewe kijiti cha kuongoza kwani and uongozi ni mchezo wa kupokezana kijiti ” amebainisha Mavunde 
Aidha Mavunde amesema kuwa Wanadodoma wanaelewa nini wanatakiwa kufanya ifikapo Oktoba 2020 juu yangu hivyo anawaachia wao jukumu la so kutekeleza haki yao ya kikatiba ipasavyo