Home Mchanganyiko Virusi Vya Corona: Papa Awataka Watu ‘Kutokubali Kushindwa Na Uoga’

Virusi Vya Corona: Papa Awataka Watu ‘Kutokubali Kushindwa Na Uoga’

0
Papa Francis amewataka watu kutosalimu amri kwa uoga wa virusi vya corona, na kuwataka kuwa “wajumbe wa uhai wakati wa kifo”.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alizungumza wakati wa sherehe za pasaka Jumamosi, katika kanisa la St Peter’s Basilica ambalo lilikuwa na watu wachache.

Waumini wa Kikatoliki bilioni 1.3 kote duniani wana fursa ya kufuatilia ibada ya moja kwa moja mtandaoni.

Marufuku ya watu kutokutoka majumbani bado inaendelezwa katika maeneo mbalimbali nchini Italia ambako kumeathiriwa vibata na janga la Corona.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte alimsifu Papa kwa kuonyesha kuchukua majukumu yake kwa tahadhari baada ya kuadhimisha ibada ya pasaka bila ya mkusanyiko wa waumini.

Wakristo kote duniani wanasherehekea sikukuu ya pasaka, moja ya sikukuu muhimu katika kalenda ya Kikikristo licha ya hatua zilizochukuliwa katika nchi nyingi duniani zilizosababisha mamilioni ya watu kusalia majumbani

Makasisi wengi wanaendesha ibada zao makanisani bila waumini kukusanyika.