Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni saba laki tano na elfu tisini na mbili (7,592,000/= )kwa watumishi wa idara ya afya halmashauri ya siha,walinzi wa shamba la miti West Kilimanjaro na shule ya sekondari Magnifikacant na mama lishe Fatuma Athumani,zilizokuwa zimedhulumiwa na kufanyiwa ubadhirifu na watuhumiwa ambao ni mhasibu wa halmashauri na mlinzi mkuu wa shamba.
Zoezi la kukabidhi fedha hizo limefanyika mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Onesmo Buswelo, akiwemo pia mtuhumiwa aliekuwa meneja wa shamba la miti West Kilimanjaro Christopha Ngonyani,watumishi waliodhulumiwa fedha zao na wahusika wote waliofujiwa fedha zao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo kamanda wa Takukuru wilaya ya Siha Deo Mtui alisema baada ya kuletewa malalamiko hayo taasisi hiyo ilianza uchunguzi ambapo baada ya kuwahoji watuhumiwa wote walikiri kufanya makosa hayo hivyo kuamuriwa kurudisha fedha hizo.
Mkuu wa wilaya ya Siha Onesmo buswelo licha ya kuipongeza TAKUKURU kwa kazi hiyo ameonekana kukerwa na kitendo hicho na kuamuru mtuhumiwa Christopha nyonyani na Namson Fisso licha ya kurudisha fedha hizo kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizo.
“Pamoja nakurudisha fedhahizo lakini watumiwa Hawa wachukuliwe hatua hatua za kinithamu ili iwefundisho kwa wengine wasijaribu kufanya vitendo Kama hivi” alibainisha buswelo
Baadhi ya wananchi na watumishi ambao walidhulumiwa fedha zao kwa hila na udangayifu wameishuruku TAKUKURU kwa kufanikisha zoezi hilo huku wakiwashauri wananchi wengine kutoogopa kuitumia taasisi hiyo
Watu waliodhulumiwa fedha zao ni watumishi 126 wa idara ya afya,walinzi 8 wa shamba la miti West Kilimanjaro,shule ya sekondari Magnificant na mama lishe Embassy Tea room zote za wilayani Siha zilizokuwa zimefanyiwa ubadhirifu na watuhumiwa Namson Fisso aliyekuwa mhasibu halmashauri ya siha na Mlinzi mkuu wa shamba la misitu la West Kilimanjaro Christopha Ngonyani.