Home Mchanganyiko WAZIRI UMMY AMEWATAKA VIONGOZI WA DINI KUCHUKUA HATUA STAHIKI ZA KUJIKINGA NA...

WAZIRI UMMY AMEWATAKA VIONGOZI WA DINI KUCHUKUA HATUA STAHIKI ZA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

0

**************************

Na Magreth Mbinga

Waziri wa afya Mhe.Ummy Mwalimu amewataka viongozi wa dini kuendelea kufanya ibada huku wakichukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Amezungumza hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano ambao umewakutanisha viongozi wa dini hapa nchini ulioandaliwa na shirika la World Vision chini ya kauli mbiu “Majukumu ya Viongozi wa Dini katika Kuzuia Maambukizi ya Corona”.

“Nyumba za ibada zichukue tahadhari kwakuwa Tanzania imetoka kwenye maambukizi ya nje na kuingia kwenye maambukizi ya ndani na waumini wajisafishe nyumbani kwao kabla ya kufika kwenye nyumba za ibada”. Amesema Mhe.Ummy.

Pamoja na hayo nae Mkurugenzi Mkuu wa shirika la World Vision Bw.Gilbert Kamanga amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika jamii dhidi ya kupambana na majanga mbalimbali Duniani.

“Viongozi wa kiimani wanajua kuwa ugonjwa wa Corona upo na wahakikishe wana elimisha na kufundisha waumini wao kuhusu ugonjwa huu na kuwapatia njia za kupambana,kuwapa moyo na matumaini kuweza kuushinda” amesema Kananga.

Sanjari na hayo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Rashidi Mfaume amezungumza kwaniaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema mkuu wa mkoa ameomba watu waendelee kupeana taarifa zilizo sahihi kutoka Wizara husika.

“Takwimu za Dunia zinasema kwa muda wa saa 24 kuna wagonjwa takribani 1,300,000 na vifo 39,275 na kwa Afrika wagonjwa 7,647 na vifo 326 wanaosema Africa hatutaguswa wanajidanganya kwa takwimu hii hali sio nzuri sana tuendelee kuchukua tahadhari ” amesema Dkt.Mfaume.

Hata hivyo Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhaji Mussa Salum amesema yupo tayari kupokea maelezo kutoka serikalini na maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya tunayazingatia lakini sio vile inavyotakiwa Jana hili ni kubwa na tunategemea sana maombi na mtu ambae sio muumini hatupatinae shida.

“Tunamshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kwa kutoka nyumba za ibada zisifungwe ili watu waendelee kumuomba Mungu atuepushe na janga hili la Corona ” amesema Alhaji Salum.