Home Michezo RONALDINHO GAUCHO AHAMISHIWA KWENYE HOTELI YA KIFAHARI KUTOKA GEREZANI

RONALDINHO GAUCHO AHAMISHIWA KWENYE HOTELI YA KIFAHARI KUTOKA GEREZANI

0

Ronaldinho Gaucho atakuwa kwenye hoteli ya nyota tano nchini Paraguay baada ya kutolewa gerezani PICHA ZAIDI SOMA HAPA

…………………………………………………………………………………………..

NYOTA wa zamani wa Barcelona na Brazil, Ronaldinho Gaucho, ametolewa gerezani na kwenda kutumikia kifungo cha nje, lakini atakuwa kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano nchini Paraguay.
Ronaldinho, bado anafanyiwa uchunguzi zaidi kwa kosa lake la kughushi hati ya kusafiria (Passport), ambapo machi 6 mwaka huu, yeye na kaka yake, waliingia Paraguay wakiwa na Passport bandia, zilizowatambulisha kuwa ni raia wa Paraguay.
Wawili hao walihukumiwa miezi sita kwenda jela, lakini baada ya kuripotiwa kulipa dhamana ya Pauni milioni 1.3, wametolewa na wataendelea kutumikia kifungo cha nje.

Ronaldinho mwenye miaka 40, atakuwa akiishi kwenye chumba cha gharama zaidi katika Hotel ya nyota tano ya Palmaroga iliyopo mji mkuu wa Paraguay, Asuncion.