Home Burudani UONGOZI WA BSS 2019 WAWEKWA KIKAANGONI

UONGOZI WA BSS 2019 WAWEKWA KIKAANGONI

0

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha Paulsen(hayupo pichani) kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anamlipa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ya Bongo Star Search kwa mwaka 2019 Bw.Meshack Fukuta, mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) Aprili 08,202 Jijini Dodoma,kulia ni Afisa Utamaduni Bw.Mfaume Said kutoka hiyo na kushoto ni Mshindi wa kwanza wa shindano la Bongo Star Search mwaka 2019 (BSS) Bw.Meshack Fukuta.

Mshindi wa kwanza wa shindano la Bongo Star Search (BSS) la mwaka 2019 yanayoendeshwa na Kampuni ya Benchmark Production Bw.Meshack Fukuta, akitoa ufafanuzi kuhusu kiasi cha pesa alicholipwa kama zawadi aliyoahidiwa kuwa ni shilingi milioni  moja na siyo milioni mbili kama inavyoelezwa katika mkutano wa Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza nawaandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 08,202 Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha Paulsen kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anamlipa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo Bongo Star Search wa mwaka 2019 Bw.Meshack Fukuta, mbele ya waandishi wa  habari (hawapo pichani) leo Aprili 08,202 Jijini Dodoma, na kushoto ni Mshindi wa kwanza wa Shindano la Bongo Star Search mwaka 2019 (BSS) Bw.Meshack Fukuta.

Baadhi ya waaandishi wa Habari wakifuatilia maelekezo ya Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza kwa Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha Paulsen (hayupo pichani) kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja  anampatia mshindi wa kwanza wa mashindano Bongo Star Search ya mwaka 2019 zawadi yake ya milioni 50 leo Aprili 08,202 Jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………………………

Na. Alex Sonna, Dodoma.

Uongozi wa Kampuni ya Benchmark Production chini ya Mkurugenzi wake Madam Rita Paulsen inayoendesha Mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki maarufu kama  Bongo Star Search (BSS) umepewa siku saba uwe umeripoti Wizara ya Sanaa, Michezo na Utamaduni ili kuweza kuweka wazi ni lini watakamilisha stahiki za mshindi wa shandano hilo wa mwaka 2019.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Sanaa,Michezo na Utamaduni Juliana Shonza leo wakati akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kupokea barua kutoka kwa familia ya mshindi huyo iliyoeleza kutokutekelezwa kwa ahadi hiyo kwa takriban miezi minne sasa ilioanisha utaratibu wa malipo hayo kuwa milioni 30 ni kwa ajili kutengeneza kazi za muziki na matangazo kwa kipindi cha mwaka mmoja na milioni 20 ni ya kukabidhiwa mkononi ambapo Mhe. Naibu Waziri amesisitiza makubaliano yote yalioanishwa kufanyiwa kazi.

Shonza amesema kuwa Kiongozi wa BSS anatakiwa kufika katika ofisi za wizara ili kujadili mpango kazi wa viongozi hao watakavyo mmaneji kijana huyo katika fedha ya kiasi cha milioni 30 ili mpango kazi huo uwezekuendana na kiasi cha fedha alizostaili kupata ikiwemo na kuangalia utaratibu wa malipo yake yatakavyo kamilishwa.

Shonza amesema kuwa maelekezo hayo yanakuja baada ya kupokea malalamiko kutoka katika familia ya mshindi huyo na kumsikiliza muhusika mwenyew ambaye hakupewa stahiki zake mpaka leo na tumejilidhisha kuwa kuna makosa ya kisheria yamefanyika na BSS waandaji wa shindano hilo.

“Baada ya kusikiliza pande zote tatu muandaji, mdhamini na mshindi BSS ndani ya siku 30 wawe wamekamilisha stahiki za kijana Meshaki Fukuta ili aweze kuendelea katika kukuza kipaji chake kwani sisi kama serikali ni kulinda haki za wasanii na kuwawezesha kufikia malengo yao katika kutafuta haki zao” ameeleza Shonza.

Shonza amesisitiza kuwa BSS ndani ya mwezi mmoja Wakifanya vinginevyo mashindano hayo yatafungiwa kama watakuwa hawajamlipa ndani ya muda huo.

Katika hatua nyingine Shonza ametoa wito kwa wa Wasanii kuwa wasikubali kufanya kazi bila mkataba ili kuwa rahisi kuweza kupata sitahiki zao kwa wakati na kuwataka BASATA kukagua mikataba ya washiriki katika mashindano kabla ya kutoa kibali cha kuendesha shindano lolote.

Lakini pia Shonza ameongeza kuwa waandaaji wa mashindano waandae zawadi za uhalisia ili kuwa rahisi kuendesha mashindano hayo ili kufanyikisha lengo la kumuinua kijana kufikia malengo yake na kuepuka changemoto kama hizi zilizo jitokeza kwa kijana Bw.Meshack Fukuta.

Naye Mshindi wa BSS 2019 Bw.Meshack Fukuta amesema kuwa amekuwa akifatilia zawadi yake yenye ghalama ya kiasi cha shilingi milioni 50 lakini hakufanyikiwa kupata kutokana na uongozi wa BSS kumpiga tarehe kila alipokwenda katika ofisi zao.

Ikumbukwe hivi karibuni changamoto kama hiyo ilijitokeza katika shindano la Miss Tanzania ambapo tatizo hilo lilipelekea mwendesha mashindano hayo kufungiwa na shindano hilo kupewa mtu mwingine