Home Burudani BASATA YAPONGEZA JUHUDI ZA WASANII KUELIMISHA JAMII KUHUSU CORONA

BASATA YAPONGEZA JUHUDI ZA WASANII KUELIMISHA JAMII KUHUSU CORONA

0

*********************************

Nawashukuru wasanii mwanzo tulipowataka watumie sanaa  kufikisha ujumbe kuhusu ugonjwa wa corona waliitikia na wakatunga nyimbo kuelimisha kuhusu ugonjwa huo.

Amezungumza hayo katibu mtendaji baraza la sanaa Tanzania BASATA Bw.Godfrey Mngereza ofisini kwake Leo jijini Dar es salaam,

Pia amesema baraza kama msimamizi wa sekta ya sanaa limewashukuru wasanii na vyombo vya habari kwaajili yakuelimisha kuhusu ugonjwa wa corona.

Vilevile amewataka wasanii kupata taarifa sahihi kutoka wizara ya afya kabla yakutoa ujumbe kwa jamii ili watoe taarifa zilizo sahihi.

“wasanii wa muziki wa asili ni vizuri zaidi kutumia lugha zao kufikisha ujumbe katika jamii husika ambao wanatumia lugha hiyo ambayo inaeleweka vizuri zaidi kwako”. Amesema Mngereza.

Aidha April 1 mwaka huu Basata walimwandikia mwanamuziki wa kizazi kipya Harmonize barua ya onyo kutokana na wimbo wake mpya wa Bedroom kukiuka maadili.

Baraza la sanaa Tanzania BASATA Linaendelea kuwakumbusha wasanii kutojidanganya kwamba wanaweza kufanya lolote, wakati wowote. Badala yake wakijite katika kuelimisha nakufanya biashara ya muziki wao.