Home Mchanganyiko MANISPAA YA ILEMELA YAONGOZA ZOEZI LA URASIMISHAJI MAKAZI NCHINI

MANISPAA YA ILEMELA YAONGOZA ZOEZI LA URASIMISHAJI MAKAZI NCHINI

0

************************

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, imefanya vizuri na kuongoza katika zoezi la urasimishaji makazi na umilikishaji wa ardhi ambapo hadi sasa imefanikiwa kuandaa michoro ya mipangomiji 58,000, kupima viwanja 52,000 na kumilikisha jumla ya viwanja 72,000.

Naibu waziri wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amepongeza viongozi wa Manispaa hiyo kwa kasi ya uendeshaji wa zoezi hilo ukilinganisha na Halmashauri nyingine nchini ambazo zimekuwa zikisuasua katika kutekeleza zoezi hilo la urasimishaji wa makazi kwa kupima na kumilikisha viwanja vichache

Moja ya wananchi waliokabidhiwa hati miliki kutoka mtaa wa Nyasaka, Bi Stella George ameishukuru Serikali na kupongeza zoezi hilo kwani litasaidia kutatua migogoro ya ardhi isiyokuwa ya lazima.

Jumla ya hati 1508 zilitolewa kwa wananchi wa Manispaa ya Ilemela na Naibu Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.