Home Mchanganyiko WAZIRI KALEMANI AFANYA ZIARA MRADI WA KUFUA UMEME WA JULIUS NYERERE MW...

WAZIRI KALEMANI AFANYA ZIARA MRADI WA KUFUA UMEME WA JULIUS NYERERE MW 2115

0

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akipokea maelezo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 Mhandisi Steven Manda jana April 5, 2020. Alipofanya ziara ya kukagua maendelelo ya mradi huo.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundo mbinu ya mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 ambapo amelidhishwa na maendeleo ya mradi huo.

Msimamizi wa mradi wa kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 Mhandisi Steven Manda akiongea na waandishi wa habari wakati wa ziara ya waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alipokwenda kutembelea maradi huo.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akitekeleza agizo la Serikali kupitia Wizara ya afya la kunawa mikono kwa sabauni na maji tiririka ili kupaamba na kuenea kwa virus covid 19 vinavyosababisha homa kali ya mapafu,kabla ya kuingia katika mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 jana April 5, 2020.

……………………………………………………………………

Na Farida Saidy Morogoro

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115  na kuridhishwa na kazi inayofanywa na mkandarasi kwa hatua aliyofikia.

Aidha Dkt Kalemani amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anakarabati barabara zote za nje na ndani ya mradi ambazo zinatumika kupitisha mizigo inayoenda kwenye mrad

Hata hivyo Dkt.Kalemani amemtaka mkandarasi huyo kumaliza kazi kwa muda ambao umepangwa kukamilisha ujenzi huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO Tito Mwinuka na msimamizi wa mradi Mhandisi Steven Manda wamewahakikishia watanzania kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati,hivyo wasiwe na shaka, kwani ukikamilika kwa mradi huo utakuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.