Home Mchanganyiko RC Wangabo atimiza ahadi yake ya kutoa magongo ya kutembelea kwa mlemavu.

RC Wangabo atimiza ahadi yake ya kutoa magongo ya kutembelea kwa mlemavu.

0

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimtaka Azla Sikazwe (aliyekaa) kuachana na gongo la alilokuwa akilitumia kutembelea ili kuweza kumpa magongo mapya.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo akimkabidhi magongo mapya Azla Sikazwe ili yaweze kumsaidia katika shughuli zake za kila siku ikiwa ni kutimiza ahadi yake ya kumsaidia magongo hayo mapya baada ya kumuahidi katika kongamano la watu wenye ulemavu lililofanyika mwezi wa pili mwaka huu wilayani Sumbawanga.

*****************************

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametimiza ahadi yake ya kutoa magongo ya kutemebelea kwa Mlemavu Azla Sikazwe Mkazi wa mtaa wa Zimamoto, Kata ya Izia, Wilayani Sumbawanga baada ya mama huyo kumuomba Mkuu wa Mkoa huo msaada wa magongo hayo wakati wa kongamano la watu wenye ulemavu lililofanyika katika Manispaa ya Sumbawanga mwezi wa pili Mwaka huu.

Mh. Wangabo amesema kuwa katika kongamano hilo lilihudhuriwa na walemavu zaidi ya 700 na kusema kuwa bado kuna wengine ambao wanahitaji msaada zaidi na hivyo kuwataka wazazi wote wenye Watoto wenye ulemavu kuhakikisha wanawaibua katika jamii pamoja na kuhakikisha wanawaandikisha shule ili kupata elimu.

“Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wetu wa Rukwa, wawaibue hawa watu wenye ulemavu hasa Watoto ili waweze kupata fursa ya kupata elimu, kwasababu wanayo haki ya kupata elimu ili waweze kulitumikia Taifa, wawaibue kokote walipo ili wawe tayari kwenda shule na sisi kama serikali tupo tayari kuendelea kuwasaidia watu wenye ulemavu, kwa kadiri itakavyowezekana,” Alisema.

Aidha, alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuwa na moyo wa kuwasaidia watu wenye ulemavu ili na wenyewe waweze kujikimu kimaisha kwani kumuwezesha ni mara moja tu ili nae aweze kujiendeleza kimaisha na hivyo wanastahili kusaidiwa.

Kwa upande wake Azla Sikazwe kwanza alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa msaada alioupata, lakini pia aliweza kumshukuru Mkuu wa mkoa kwa moyo wake wa huruma uliomuwezesha kumsaidia magongo hayo ambayo yatamrahisishia kufanya mizunguko katika shughuli zake mbalimbali za kiujasiliamali.

“Muheshimiwa hapa nimekuja, kweli nashukuru hata sijui niseme nini lakini yote nayaacha mikononi mwa Mungu, na nimekuja mimi ni mjasiliamali lakini, sina chochote hata kuja kwangu nimeomba tu ridhaa kwa mtu ndio akanileta hapa,” Alimalizia.

Katika makabidhiano hayo pia alikuwepo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Rukwa Ndugu Maria Kalula amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kitendo hicho cha kuweza kumsaidia mama huyo vifaa hivyo ili aweze kufanya shughuli zake na kusisitiza kwa wazazi wote wanaowaficha Watoto walemavu kuacha kitendo hicho na badala yake wajitokeze ili waweze kupatiwa msaada.

“Tendo ambalo amelifanya mkuu wetu wa mkoa nit endo la kihistoria kwakweli, na tunamshukuru sana kwasababu ameona umuhimu wa kuwahudumia walemavu, ni kweli walemavu wako wengi wengine hata bado hawajaanza kutokeza wamefishwa ndani, mi natoa ushauri kwa wale ambao wana Watoto wa aina hiyo, waweze kuwatoa ndani wawatambulishe kwa serikali yetu sikivu, na Mkuu wa Mkoa ameanza naamini ataendeleza hili jambo ili aweze kuwasaidia na wengine,” Alisema.