Home Mchanganyiko RC NDIKILO ASITISHA MKUTANO WA KANISA LA EFATHA KUJIKINGA NA UGONJWA WA...

RC NDIKILO ASITISHA MKUTANO WA KANISA LA EFATHA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA

0

*****************************

6,april
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKUU wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo, asitisha mkutano wa Kanisa la Efatha uliokuwa ufanyike kuanzia tarehe 7 april hadi 12  aprili mwaka huu, Bungu Wilayani Kibaha ikiwa ni tahadhari ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona Mkoani hapa.
Akitembelea eneo la Mkutano  huo akiwa na Kamati ya Usalama Mkoa alipokea taarifa ya maandalizi ya mkutano huo ikiwa na namna walivyojipanga kuchukua tahadhari ya maambukizi ya COVID 19.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Vivian Mmari alibainisha ,mkutano huo ni wa siku tano na  utajumuisha washiriki 3,000 ambao ni Viongozi  wa Mikoa wa kanisa hilo kutoka kote Nchini,na kusema wamejipanga kujikinga na maambukizi ya Covid 19 ikiwa ni pamoja na kufanya vipimo vya awali ,na kuwa na vitakasa mikono kila eneo.
Baada ya kupokea taarifa hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa Mhandisi Ndikilo, alieleza kwa “Mazingira waliyoyakuta Wingi wa watu, Mazingira ya kulala,  Mwingiliano wa watu kutoka Mikoa mbali mbali, Idadi ya siku za mikutano Kamati ya Usalama Mkoa inatilia shaka kukiukwa kwa maelekezo ya Serikali yaliyotolewa  ya  kuchukua tahadhari na kuepuka Mikusanyiko isiyokuwa na lazima”
Aidha aliongeza kuwa Lengo sio kuzuia ibada ni kuchukua tahadhari madhubuti ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona unaoenea kwa kasi.
Licha ya hayo,Mhandisi Ndikilo alisisitiza ,waumini wamadhehebu yote  Mkoa wa Pwani waendelee na ibada kwa siku zao za ibada huku wakichukua tahadhari.