………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mbunge wa Konde (CUF) Khatib Said Haji amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumchukulia hatua Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Mhe.Salama Aboud Talib aliyekataa kukaa kwenye karantini na kusababisha maambukizi ya virusi vya Covid-19 kwa watu wawili kwenye familia yake.
Kauli hiyo ameitoa bungeni leo wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021,Mhe.Haji amesema kuwa matokeo ya nyumbani kwake kuna watu wawili waamepata Virusi vya Corona pia huko hospitali haijulikani matokeo yake nini.
“Ndani ya siku tatu ameng’ang’ana kukaa hospitali ya Mnazi Mmoja matokeo yake akatolewa kwa nguvu baada ya kuona jambo hili limekuwa kubwa nipo alikubali kuwekwa kwenye karantini,”amesisitiza Mhe.Haji
Aidha Mhe.Haji amesema kuwa alifanya hayo kutokana na kiburi cha madaraka yake na pia amempongeza makamu wa pilli wa Rais Zanzibar kwa kukubali kukaa karantini alipotoka nje ya nchi bila kulazimishwa.