Home Michezo YANGA YATEUA VIGOGO WANNE WAPYA

YANGA YATEUA VIGOGO WANNE WAPYA

0

……………………………………………………………………….

KAMATI  ya Utendaji ya Klabu ya Yanga leo Aprili 3, 2020 chini ya Mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla imewateua  Suma Mwaitenda na Haruna Batenga kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji kujaza nafasi zilizoachwa baada ya wajumbe wawili wa kuteuliwa kujiuzulu.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, pia Hamad Islam ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, na Dominic Albinus kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi.