Home Mchanganyiko Maziko ya Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Misungwi

Maziko ya Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Misungwi

0
Mzee Clement Hayahaya na mkewe wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao marehemu Simeon Hayahaya,aliyekuwa Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Misungwi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli (kushoto) jana, akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Simeon Hayahaya,kulia ni Mjumbe wa NEC Taifa Paul Bundala. 
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mwanza, Hellen Bogohe akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Siasa na Uenezi wa Wilaya ya Misungwi, Simeon Hayahaya.
Baba mzazi wa marehemu Simeon Hayahaya, Mzee Clement Hayahaya akisaidiwa kwenda kuweka udongo kwenye kaburi la mwanaye jana.
Viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Mwanza na wilaya  wakiwa kando ya jeneza la marehemu Simeon Hayahaya.Kutoka kushoto wa pili ni Katibu wa CCM Mkoa, wa Mwanza, Salum Kalli.
Paroko wa Parokia ya Buhingo, Padri Kelvin Onesmo Mkama (aliyefunga kiunoni) wakati ya ibada ya mazishi ya Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Misungwi, Simeon Hayahaya jana.

Mke wa marehemu Simeon Hayahaya, Magreth Zugamawe (mbele)  akisaidiwa kwenda kutoa heshima za mwiaho kwenye jeneza lililobeba mwili wa mumewe. Picha zote na Baltazar Mashaka