Home Mchanganyiko WANANCHI WA KIMARA BARUTI NA MAKOKA KUNUFAIKA NA AJIRA KWENYE UJENZI WA...

WANANCHI WA KIMARA BARUTI NA MAKOKA KUNUFAIKA NA AJIRA KWENYE UJENZI WA DARAJA LA MTO GIDE

0

******************************

Na Magreth Mbinga

Mkandarasi wa Ujenzi wa daraja la mto Gide katika kata ya Kimara Baruti ametakiwa kutoa ajira kwa wananchi wa eneo hilo ili kuweza kuwanufaisha wakazi hao.

Amezungumza hayo Diwani wa kimara baruti Mh Pasco Manota wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo wakati akiwapa maelekezo kuhusu kuanza ujenzi wa daraja hilo.

Pia amesema Halmashauri imetoa milioni 200 na TARURA imetoa malioni 100 kwaajili ya mchango wa ujenzi wa daraja hilo la mto Gide.

Vilevile mkandarasi anaetarajia kujenga daraja hilo Nevablack Mwakalinga emesema wanatarajia kuanza ujenzi rasmi jumatatu na amepewa muda wa miezi mitatu lakini wanatarajia kufanya kazi kwa muda wa miezi miwili kama mvua haitanyesha kwa wingi.

“Daraja litakuwa na urefu wa mita kumi na moja na litakuwa la njia mbili ambalo lita ghalimu kiasi cha milioni 321 litakalo weza kupitisha magari ya uzito wa tani kumi” amesema Mwakalinga.

Sanjari na hayo Mwajuma Mnugila mwananchi wa eneo hilo la Baruti amesema anapongeza serikali kwa jukumu kwa hatua waliochukua ya kujenga daraja hilo kwakuwa wamepoteza ndugu zao wengi katika mto huo.

“Wauangalie mto huu kabla ya kuanza ujenzi na waangalie njia yake ya zamani ili waweze kuurudisha ndipo waendelee na ujenzi wa daraja hilo” amesema Mnugila.

Hata hivyo Juma Hoza mkazi wa eneo hilo amewataka wananchi kuhama bondeni ili kujihadhari na majanga yatokanayo na kukaa eneo hilo na amemtaka mkandarasi kujenga kwa wakati ili waendelee na shughuli za kila siku.

“Daraja hili watoto wetu wanavuka kwenda upande wa pili kufata elimu na wajawazito pia hutumia njia hiyo kwenda hospitali na wengine hujifungulia eneo hilo” amesema Hoza.

Mwenyekiti wa mtaa wa baruti Mohammed Kilongo amesema Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kusikia kilio chake kwakuwa ujenzi wa daraja hilo ni moja kati ya ahadi yake katika kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2015.