Home Mchanganyiko PROF.NYANTAHE APOKEA KITABU CHA “MAKING AFRICA WORLD’S LARGEST ECONOMY” KUTOKA KWA MWANDISHI...

PROF.NYANTAHE APOKEA KITABU CHA “MAKING AFRICA WORLD’S LARGEST ECONOMY” KUTOKA KWA MWANDISHI DERIK MURUSURI

0

Mhandisi Dkt Samuel M. Nyantahe, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) akipokea Kitabu cha ‘MAKING AFRICA WORLD’S LARGEST ECONOMY,’ kutoka kwa mwandishi wake, Ndg Derek Murusuri, leo jijini Dar es Salaam.

**********************************

Dk Nyantahe ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Daima Associates Limited, ni miongoni mwa wahadhiri waanzilishi wa Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mhandisi Dkt Nyantahe pia, katika uongozi wa Mwalimu Nyerere, aliwahi kusimamia mradi wa kuzalisha magari (State Motor Corporation) ambapo Tanzania ilishirikiana na makampuni mbalimbali ya nje kuunda magari yao hapa nchini na kuyasambaza katika mataifa mengine ya Afrika.

Baadhi ya makampuni hayo ni SAAB SCANIA, LANDROVER. ISUZU NA HONDA. Kitabu alichokabidhiwa, kinahamasisha mawasiliano ya sayansi katika kuimarisha ujenzi wa uchumi wa viwanda Afrika.