Home Mchanganyiko SIWATISHI, CORONA INAUA-RC.MAKONDA

SIWATISHI, CORONA INAUA-RC.MAKONDA

0

*****************************

Na Magreth Mbinga

Tusicheze na uhai wa binadamu tuwe sehemu ya serikali katika kuokoa maisha ya Watanzania katika kupambana na janga hili la virusi vya corona.

Amezungumza hayo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda katika ziara yake ya kukagua uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuangalia utendaji wa kazi na ukaguzi wa abiria wanaoingia nchini.

“Ndege kabla haijawasili uwanjani inakuwa na mawasiliano na uwanja husika kama kuna abiria anachangamoto waweze kumpatia msaada mapema afikapo uwanja wa ndege” amesema Makonda.

Pia Makonda amesema kunawatu hawapendi kunawa mkono mara kwa mara kwaajili ya kujikinga na virusi vya corona ili visisambae kwa haraka endapo watanawa mikono kwa sabuni na maji yanayo tiririka.

“Tunamshukuru Mungu mpaka sasa hakuna sababu ya kuogopa kinachotakiwa kujikinga ili usipate maambukizi ya virusi vya corona lakini tuendelee kufanya kazi kama kawaida huku tukichukua taadhali” amesema Makonda.

Hatahivyo amesema Leo asubuhi Kuna zaidi ya abiria mia mbili walitakiwa waende Comoro lakini wameshindwa kwenda kwa sababu nchi hiyo imesitisha kuingia wageni kutoka nje ni kwaajili ya kujikinga na virusi hivyo.

Sanjari na hayo Makonda amesema idadi ya wageni wanaotoka nje ya Tanzania imepungua kwa sababu ndege iliyokuwa inabeba abiria 250 kwasasa inabeba abiria 20 ambayo ni zaidi ya asilimia themanini.

Makonda amemalizia kwa kusema waandishi wa habari ni muhimu sana katika kupambana na virusi vya corona kwani wao ni daraja kati ya wananchi na serikali kwa kupitia wao wananchi wanapata elimu.