Home Mchanganyiko Ujenzi wa Maabara changamano Utasaidia, Kuimarisha Afya na Usalama wa Wananchi

Ujenzi wa Maabara changamano Utasaidia, Kuimarisha Afya na Usalama wa Wananchi

0

Picha ya pamoja ya Viongozi Mbali Mbali waliohudhuria Hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika makoa Makuu ya tume ya Nguvu za Atomik jijini Arusha.
*******************************
Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako  amesema Ujenzi wa Maabara  changamano katika Tume ya Nguvu za Atomik Tanzania  ni sehemu ya Juhudi na Mipango ya Serikali katika kuimarisha afya na  Usalama wananachi na mazingira kwa ujumla.
Pia ndalichako alisema kuwa Maabara itakapokamilika itaongeza ufanisi  wa kufanya tafiti Mbali Mbali katika sayansi ya nyuklia  ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbali Mbali za kiuchumi,kijamii na kiusalama.
 Katika Hatua nyingine amezitaka  Taasisi zote zilizopo chini ya Wizara hiyo kuhakikisha wanatekeleza agizo la serikali katika kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya homa ya Corona kwa kuweka huduma muhimu za tahadhari kwa wananchi wanaofika katika taasisi hizo kupata huduma.
Akizungumza Jijini Arusha katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya kisasa ya awamu ya pili, itakayo shughulika masuala ya mionzi na upimaji wa sampuli mbalimbali ikiwemo za chakula.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametumia fursa hiyo kumueleza Waziri huyo kuwa mkoa wa Arusha Upo Imara katika kuhakikisha kuwa inashughulikia Usalama wa wananchi wake.
Naye  Mkurugenzi mkuu wa tume ya Nguvu za Atomiki nchini Profesa Lazaro Busagala alisema kuwa Serikali ilianzisha mradi wa kujenga  maabara changamano ya kisasa katika Makao Makuu ya time ya atomik iliyopo  hapa jijini Arusha ,kwa lengo la kuongeza uwezo wa usimamizi na usimamiza wa  Nguvu za Atom hapa nchini.
Aidha Profesa Busagala alisema katika kuongeza uwezo huo Serikali iliona umuhimu wa kuwa na maabara changamano ya kisasa  yenye uwezo wa kiuchunguzi ili kuimarisha usimamizi wa uchunguzi wa urine pale yatakapoanza kuchimbwa pamoja na kuboresha huduma za maabara ili kulinda wananchi na Mazingira dhidi ya matumizi yasiyo salama kwa teknolojia za nyuklia na kuongeza wigo, wa Mafunzo ya vitendo kwa programu za sayansi na teknolojia ya nyuklia hapa nchini.
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Ili anzishwa kwa sheria ya bunge namba 7 ya mwaka 2003 ikiwa na majukumu ya kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini.