Home Burudani MWANA FA AMEKUTWA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

MWANA FA AMEKUTWA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

0

**************************

NA EMMANUEL MBATILO

Msanii wa kizazi kipya @mwanafa, amepima na kugundulika na maambukizi ya virusi vya Covid 19 maalufu Corona na sasa yupo kwenye uangalizi na sasa anaendelea vizuri.

“Majibu ya vipimo vyangu vya Covid 19 yamerudi chanya. Inaudhi.Siumwi kabisa. Nipo sawa 100%.Na nimejitenga toka niriporudi kuepuka kuathiri wengine”. Amesema @mwanafa.

Aidha @mwanafa amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kadri ya uwezo wao kukwepa na maambukizi hayo.