Home Mchanganyiko BUNGE LASITISHA KUPOKEA WAGENI WANAOKUJA KUJIFUNZA

BUNGE LASITISHA KUPOKEA WAGENI WANAOKUJA KUJIFUNZA

0

***************************

Ofisi ya Bunge inapenda kuutangazia umma kwamba kuanzia sasa imesitisha utaratibu wa kupokea wageni mbalimbali wakiwemo wanafunzi wanaokuja Bungeni
kwa lengo la kuona au kujifunza shughuli za Bunge.

 

Wageni watakaoruhusiwa kuingia Bungeni ni wale wenye kazi na vibali maalum tu. Hatua hii ni moja ya mikakati ya Bunge iliyotangazwa na Mheshimiwa Spika Job Ndugai (Mb) ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

 

Hivyo,tunawaomba wadau mbalimbali kusitisha maombi ya kutembelea Bunge hadi hapo itakavyoelekezwa vinginevyo.