Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu akizungumza jambo kuhusiana na mikakati ya serikali ya awamu ya tano ya kuweka mipango ya kuunganisha nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda vipya 50 wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini ambayo ilifanya ziara yake ya kikazi ya kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo katika Wilaya ya Mkuaranga.(Picha na Victor Masangu)
Baadhi ya wabunge wanaounda kamati ya nishati na madini wakati wanaingia katika kiwanda cha kuzalishia chuma cha Lodhia ikiwa ni moja ya ziara yao ya kikazi kwa ajili ya kuijionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na wawekezaji pamoja na kubaini changamoto zao, wa kati kati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.(Picha na Victor Masangu)
Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda cha Lodhia ambacho kinajishighulisha na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo chuma, akiwaonyesha wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na madini jinsi ya kiwanda hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuwaelezea changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuziwasilisha kwa serikali zifanyiwe kazi.(Picha na Victor Masangu)
Mwonekano wa mtambo maalumu wa kuzalishia nishati ya umeme wa gesi asilia ambao umefunngwa na shirika la TPDC katika kiwanda hicho cha kuzalishia chuma pamoja na kutengenezea mabomba ya maj wakati wa ziara hiyo ya kamati ya bunge ya nishati na madin.(Picha na Victor Masangu)
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na madini wakiwa na viongozi mbali mbali wa kiwanda hicho wakitembezwa katika maeneo mbali mbali ili kuweza kujionea mwenendo mzima wa vyuma chakavu vinavyoyayushwa na kutengenezwa Nondo mpya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ikiwemo ile ya serikali.(Picha na Victor Masangu)
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Lodhia Haruni Lodhia ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa kutengeneza Nondo
*************************
VICTOR MASANGU, MKURANGA
Naibu Waziri wa nsihati Subira Mgalu alisema kwamba katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 serikali imedhamilia kusambaza na kuwaunganishia nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda vipya vipatavyo 50 ambavyo vimepitiwa na bomba la gesi ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam Pwani pamoja na Mtwarana kuongeza gharama za umeme zitashuka pindi mradi wa bwawa la umeme mwalimu nyerere utakapomalika Juni 2022 na kuzalisha mega wati 2115.
Mgalu aliyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini ambayo yameifanya kwa lengo la kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ambavyo vinajiendesha kwa kutumia nishati ya umeme ikiwa pamoja na kuzungumza na wawekezaji ili kubaini changamoto wanazokabiliana nao na kuzitafutia ufumbuzi.
Naibu Waziri huyo alibainisha kwamba kwa sasa serikali ya awamu ya tanoi mpango wake mkubwa ni kuhakikisha inasambaza na kuviunganishia viwanda mbali mbali nishati ya umeme ili viweze kutimiza malengo ya azma y serikali ya kuwa na uchumi wa kati pamoja na kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana ambao ni wazalendo lengo ikiwa waweze kujikwamua na wimbi la umasikini.
“Mpango wetu wa serikali licha ya kuwa bado kuna baadhi ya maeneo ya viwanda hayajafikiwa na nishati ya umeme lakini kwa sasa kupitia nishati ya gesi asilia tuna mpango wa kuviunganishia viwanda vipya vipatavyo 50 ambavyo vipo katika Mikio ya Dar es Salaam, Mtwara pamoja na Mkoa wa Pwani hivyo juhudi za makusudi bado zinaendelea kwa hiyo viwanda ambavyo vinapitiwa na bomba kubwa la gesi vitaweza kunufaika.
Aidha Naibu Waziri huyo alifafanya kwamba pindi mradi wa umeme wa bwawa la Malimu Nyerere uliopo Wilayani Rufiji utakapokamilika utaweza kuwa ni mombozi mkubwa kwa wawekezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa kutoka maenne mbali mbali sambamba na kuwaunganishia wananchi wengine pamoja na taasisi za serikali na sizozo za serikali.
Katika hatua nyingine Mgalu ameipongeza kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini kwa kuweza kwenda kutembelea katika kiwanda cha kuzalisha chuma pamoja na mabomba ya maji ili kuweza kubainichangamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wawekezaji na hatimaye kuweza kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambao utasaidia kutimiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda hivyo.
Kwa upande wake Kaimu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini Vedastus Matayo alibainisha kwamba ujenzi wa kiwanda hicho utaweza kuipunguzia serikali gharama kubwa ambazo zimekuwa zikitumia kwa ajili ya kuagiza baadhi ya Nondo kutoka nje ya nchi hivyo amempongeza mwekezaji huyo kwa kuwekeza katika Wilaya ya Mkuranga kwani kumesaidia vijana zaidi ya 1 300 kupata fursa ya ajira.
“Sisi kama kamati kwa kweli tunapenda kumpongeza mwekezaji huyo kwa kuweza kuwekeza katika Wilaya ya Mkuranga ambayo ipo katika Taifa letu ya Tanzania hii ni hatua nzuri ambayo ameifanya na kwa sasa anazalisha bidhaa mbali mbali kwa kutumia nishati ya umeme wa gesi asilia hivyo kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wenyewe pamoja na wale wawekezaji wa ndani na nje ya nchi,”alibainisha Matayo
Aidha Matayo katika hatua nyingine alibainisha kuwa Kamati ya bunge ya nishati ya kudumu ya nishati na madini ilibaini kuwepo kwa urasimu na ucheleweshaji wa vibali kutoka kwa baaadhi ya mamlaka zinazohusika kwa wawekezaji wa sekta ya viwanda pamoja na gharama ya nishati ya umeme kuwa ni kubwa hivyo hivyo watayachukua mapendekezo hayo kwa ajili ya kuyawasilisha bungeni ili serikali iweze kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.
Pia alisema kuwa mapendekezo pamoja na changamoto mbali mbali ambazo wamekutana nazo katika kiwanda hicho ikiwemo na maeneo mengine ambayo tayari wameshayapitia watayawasilisha serikalini ili yaweze kufanyiwa kazi ikiwemo na kutilia mkazo katika suala la usumbufu mkubwa wanaoupata wawekezaji pindi wanapohitaji kuagiza matilio mbali mbali kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zao.
Awali akitoa taarifa mbele ya Kamati ya nishati na madini Mkurugenzi mtendajiwa wa kiwanda hicho cha kuzalisha chuma Haluni Lodhia amebainisha kwamba hapo awali walikuwa wanakabilia na changamoto kubwa ya ukosefu wa nishati ya umeme wa uhakika pamoja na miundombinu ya barabara,ambapo ameipongeza serikali ya awamu ya tano kupitia Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa litafutia ufumbuzi suala hilo na hatimaye kuanza utekelezaji wa kuzalisha bidhaa mbali mbali, ikiwemo Nondo, mabomba ya maji na bodi za jasi.