Home Mchanganyiko IGP SIRRO TUMEJIPANGA KUKABILIANA NA UHALIFU

IGP SIRRO TUMEJIPANGA KUKABILIANA NA UHALIFU

0

***************************

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema Jeshi la Polisi limejipanga vizuri katika kuhakikisha linakabiliana vyema na matukio ya uhalifu yanayojitokeza nchini na kwamba Jeshi lipo imara hasa kipindi hiki cha
kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

 

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akikamilisha ziara yake ya ukaguzi katika Kanda Maalum ya Polisi Jijini Dar es salaam kwa kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, ambapo amewataka askari wa vyeo mbalimbali kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria.

 

Kuhusu Corona, IGP Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi limechukua hatua madhubuti ikiwemo kutoa elimu kwa askari wa vyeo mbalimbali na wateja wanaofika kupata
huduma katika vituo vya Polisi kuhusu kujikinga ili kuendelea kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona.