Home Mchanganyiko WANAOISHI MABONDENI MUHORO NA CHUMBI WAONDOKE KUJINUSURU NA MAAFA YA MVUA-RC NDIKILO

WANAOISHI MABONDENI MUHORO NA CHUMBI WAONDOKE KUJINUSURU NA MAAFA YA MVUA-RC NDIKILO

0

*******************************

NA MWAMVUA MWINYI,RUFIJI
MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ameagiza, wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni ambayo yana athari kubwa kwa mvua ,huko Muhoro na Chumbi ,wilayani Rufiji kuhamia maeneo ya yaliyo salama kwako ili kujiepusha na maafa na madhara makubwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Amesema ,hadi sasa maafa tayari ni makubwa na takwimu zilizofika mkoani hadi sasa ni takriban hekta 6,600 za mashamba na makazi ya watu zimeathirika ,kituo cha afya kimezingirwa na maji hakitoi huduma pamoja na kaya 3,500 zimekumbwa na maafa hayo.
Ndikilo alitoa kauli hiyo, baada ya Mwenyekiti wa kijiji cha Muhoro Magharibi ,Amin Mnyimwa wakati akitoa kilio na kutubu mafuriko yalivyowaathiri na kukubali wahamishwe maeneo mengine ili kunusuru maisha yao.
Ndikilo alieleza, kutokana na athari hiyo kamati ya ulinzi na usalama mkoa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)kimelazimika kwenda kujionea hali halisi ya majumba ,mazao mbalimbali kuzama katika maji.
Alisema, serikali inafanya juhudi za kuwahamisha na kukamilisha taratibu ya kuzungumza na wakala wa misitu (TFS) ambayo ipo chini ya  wizara ya maliasili na utalii.
“Mababu walioishi maeneo haya tangu miaka ya 1978 walikataa kuhama, vizazi vyao ndio hivi vinavyopata madhara sasa ,”Ni lazima muhamie maeneo ya juu na tunakamilisha majadiliano na wizara hiyo husika.”
“Wilaya na halmashauri ianzeni kupata idadi ya wakazi husika waliopata madhara wapate ardhi ya maeneo ya kudumu na inapaswa kutengwa hekari 30 ya kituo cha afya na hekari 20 itengwe kwa ajili ya shule”alielezea Ndikilo.
Mkuu huyo wa mkoa ,alifafanua, wataangalia namna ya kuhamisha shule na kituo cha afya kwenye eneo hilo litakalotengwa na TFS.
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Rufiji,Juma Njwayo alithibitisha kuwa, eneo hilo halifai kuishi kabisa pia wapo waliojenga ndani ya mita 60.
Awali mwenyekiti wa Muhoro Magharibi ,Mnyimwa alisema, hadi sasa wanafunzi wa sekondari 303 wa maeneo ya Muhoro Magharibi wamehamishiwa sekondari ambapo wazazi wanatakiwa kuchangia unga kilo nane,sukari kilo mbili,maharage kilo mbili ambazo hazitoshi.
Alisema ,wapo tayari kuhama maeneo waliyopo ili kujiepusha na kero wanayoipata sasa.
Nae mwenyekiti wa kijiji cha Muhoro, Muharami Mkumba alibainisha, kijiji hicho kina vitongoji vinne kati yake vitatu vimekumbwa na adha ya maji na kaya 580.