Home Michezo Bluefins yatwaa  ubingwa kuogelea ya  Mwanza

Bluefins yatwaa  ubingwa kuogelea ya  Mwanza

0

Waogeleaji wa klabu ya Bluefins wakishangilia baada ya kushinda mashindano ya kuogelea ya Mwanza yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Isamilo.

**************************

Dar es Salaam. Klabu ya Bluefins ya Dar es Salaam imefanikiwa kunyakua ubingwa wa mashindano ya kuogelea ya mkoa wa Mwanza yajulikanayo kwa jina la Isamilo swimming championships.

Kwa ushindi huo, Bluefins inakuwa klabu pekee Tanzania kufanikiwa kutwaa ubingwa mara mbili katika mashindano matatu yaliyokwisha fanyika mpaka sasa kwa mujibu wa kalenda ya mashindano ya mwaka huu iliyotolewa na Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA).
Bluefins awali ili nyakua ubingwa wa mashindano ya Morogoro (Mis Piranhas) na baadaye kumaliza katika nafasi ya pili katika mashindano ya Taliss-IST yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya waogeleaji 200 kutoka klabu 10, Bluefins ilikusanya jumla ya pointi 3,031.5 na kufuatiwa na wenyeji, Mwanza waliojikusanyia pointi 2,932.5.

Kwa upande wa wavulana, Bluefins ilinyakua nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 1,500 na kufuatiwa na Mwanza iliyopata pointi 1,209.

Mwanza ilishika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake baada kwa kupata pointi 1,493.5 na kufuatiwa na Bluefins kwa kukusanya pointi 1,341.5.

Klabu ya Bluefins ilifanikiwa kushinda jumla ya medali 93 ambapo kati ya hizo, 28 ni dhahabu, 31 za fedha na 34 za shaba.

Kocha Mkuu na Muasisi wa klabu hiyo,  Rahim Alidina aliwapongeza wachezaji wake kwa bidii waliyoifanya na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo.

 “Tumefarijika sana na matokeo ya Mwanza ambayo yameendelea kuipa sifa klabu katika mchezo wa kuogelea. Mara ya kwanza tulitwaa ubingwa mwaka 2016 na kufanikiwa kurejesha ubingwa wetu,” alisema Alidina.

Alisema kuwa bado tunaendelea kuwanoa waogeleaji wetu ili kuendelea kufanya vyema katika mashindano ya ndani nan je ya nchi.

Mbali ya Bluefins na Mwanza, klabu nyingine zilizoshiriki katika mashindano hayo ni Braeburn, Dar Swim Club, FK Blue Marlins, Geita Gold Mine International, Lake, Taliss-IST, Tanzania Latham Swim Club na UWCEA  ya Moshi.