Home Mchanganyiko VIJIJI 9,009 VYASAMBAZIWA UMEME NCHINI

VIJIJI 9,009 VYASAMBAZIWA UMEME NCHINI

0

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye shati la bluu-katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kijiji Buhungu, kata Kigongo, Wilaya ya Chato , Mkoa wa Geita wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi za usambazaji umeme vijijini Machi 13 mwaka huu.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye shati la bluu) akizungumza na wananchi wa kijiji Buhungu, kata Kigongo, Wilaya ya Chato , Mkoa wa Geita wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi za usambazaji umeme vijijini Machi 13 mwaka huu.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye shati la bluu) akicheza kwa furaha na baadhi wananchi wa kijiji Buhungu, kata Kigongo, Wilaya ya Chato , Mkoa wa Geita wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi za usambazaji umeme vijijini Machi 13 mwaka huu.

Wananchi wa kijiji Buhungu, kata Kigongo, Wilaya ya Chato , Mkoa wa Geita, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi za usambazaji umeme vijijini Machi 13 mwaka huu.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye shati la bluu) akikata utepe kuashiria kuwashwa kwa umeme katika kijiji cha Buhungu, kata Kigongo, Wilaya ya Chato , Mkoa wa Geita wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi za usambazaji umeme vijijini Machi 13 mwaka huu.

*****************************

Hafsa Omar-Geita

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amesema kazi ya usambazaji umeme vijijini nchini inaendelea kwa kasi ambapo mpaka sasa takribani vijiji 9,009 tayari vimesambaziwa umeme.

Aliyasema hayo, tarehe 13 Machi, 2020 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuwasha umeme katika kijiji cha Buhungu, Kata ya Kigongo,Wilaya ya Chato, mkoani Geita.

Alisema kuwa, Serikali itahakikisha inapeleka umeme katika vijiji vyote 12,268 vilivyopo nchini katika muda uliopangwa na haitaruka kijiji hata kimoja.

“ Kwa sasa kuna wilaya 35 ambazo vijiji vyake vyote vina umeme na tutafanya hivyo katika wilaya zote za nchi yetu na ndani ya miaka hii miwili ni matarajio yetu itafika mahala katika wilaya zote usikute kijiji ambacho hakijafikiwa na umeme.” Alisema.

Akieleza baadhi ya manufaa ya usambazaji umeme vijijini, alisema ni pamoja na uwepo wa nguvu kazi ya vijana ambao watabaki vijijini kufanya shughuli za kiuchumi na wananchi kupata huduma bora zinazotokana na umeme kufika katika sehemu zinazotoa huduma za kijamii kama visima vya maji, vituo vya afya, shule n.k

“Manufaa makubwa yameanza kuonekana kwasababu vijiji kwa sasa vimeshakuwa na sehemu maalum ambazo watu wanafanya shughuli za kiuchumi kwahiyo miji nayo inahamia vijijini lakini manufaa makubwa ni nguvu kazi ya vijana kwa sasa kubaki vijijini na kufanya shughuli za maendeleo.” Alisema Dkt.Kalemani

Aliongeza kuwa, manufaa makubwa ya uwepo wa umeme ni kuongezeka kwa viwanda nchini ikiwemo katika maeneo ya vijijini, ambapo takwimu zinaonesha kuwa kuna zaidi ya viwanda 55,000 vinavyotokana na jitahada za Serikali za kusambaza umeme vijijini na kwenye Miji.