Home Mchanganyiko KAMATI YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA...

KAMATI YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA YASISITIZA VIWANGO VYA UBORA

0

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, akijaribu ubora wa mataruma yanayotengenezwa katika Kiwanda cha Mataruma Kilosa, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR,
Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi
Machibya Masanja, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea na kukagua mataruma yanayozalishwa katika Kiwanda cha Kilosa, Mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (wa pili kushoto) akiwa na wajumbe wa kamati hiyo,wakimsikiliza Mhandisi wa
Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Ezekiel Abel, akitoa maelezo ya namna kiwanda cha mataruma Kilosa kinavyozalisha mataruma, wakati
kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani
Kakoso (wa pili kulia) na wajumbe wa kamati hiyo, wakati ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, na moja ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Charles Kitwanga, ndani ya treni ya majaribio ya SGR, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara na Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika mlango wa tanuru la reli, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Sehemu ya Makutupora-Dodoma, Mkoani Morogoro.