Home Mchanganyiko VIJANA WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI VYA KUZALISHA MATUNDA MKOANI MARA

VIJANA WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI VYA KUZALISHA MATUNDA MKOANI MARA

0

Vijana waliohudhuria kongamano la fursa katika kilimo lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kanisa Katoliki  wilani Butiama wakimsikiliza kwa makini  muwezeshaji wa dawati la mikopo kutoka benki ya NMB kutoka wilaya ni Bunda

Mgeni Rasmi  katika kongamano la vijana  Mhe. Adamu Malima  Mkuu wa Mkoa wa Mara akihutubia wakati 
wa kufunga kongamano hilo lililodumu kwa sikumbili mfululizo.

Makamu mwenyekiti wa kongamano Dkt. Zakariya Muyengi akifananua jambo wakati wa kongamano hilo

*****************************

Na Bashiri Salum
Butiama

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adamu Malima amewataka vijana kujiunga katika vikundi na kuzalisha kwa wingi matunda kwa kuwa mahitaji yake ni makubwa ndani na nje ya nchi.

Hayo ameyasema hivi karibuni wakati wa kufunga kongamano la vijana wakulima lililofanyika kwa siku mbili mfululizo katika ukumbi wa kanisa Katoliki Wilaya ya Butiama Mkoani humo.

Akitolea mfano kampuni ya Bakharesa iliyopo Jijini Dar es salaam na Jambo iliyopo mkoani Shinyanga amesema makampuni hayo yapo tayari kuingia mkataba na wakulima wa matunda hivyo vijana wametakiwa kutumia fursa hiyo.

Mhe. Malima ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa hatua za kubainisha fursa za kilimo mifugo na uvuvi kwa wakulima vijana kupitia makongamano yanayoendelea kufanyika katika kanda mbalimbali hapa Nchini.

Aidha amesema kwamba serikali ya mkoa itatoa ushirikiano mkubwa kwa vijana ikiwemo kuwapatia ardhi ya kulimo mifugo na uvuvi ambapo kikundi na aridhi vitaendelea kuwa mali ya Kijiji.

Katika hatua nyinge Mhe. Malima ameliomba shirika la SUGECO (The Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative) kuandaa utaraibu kwa kushirikiana na Hamlashauri husika elimu ya vitendo katika Halmashauri ili kupunguza gharama za wakulima kufuata Kamba atamizi zilizopo mkongo wilayani Rufiji mkoa wa pwani kwa mafunzo.

’Hapa kuna wakulima Zaidi ya 250 kama wote wakishawishika watatakaiwa kuwafuta SUGECO walipo ili kufanya kazi kwa vitendo kwa muda mrefu, hili sio sawa , shirika hili liandae utaratibu kwa kushirikiana na Halmashauri zetu wapate eneo wao ndio wawafuate wakulima’. Alisema Mhe. Malima.

Kabla ya kufunga kongamano hilo aliwataka vijana kushiriki ufugaji wa nyuki ambao utasaidia kutunza mazingira kwa kupanda miti stahiki ambapo vijana hao watapata kipato na uchumi wa taifa utakuwa Zaidi.